Wednesday, 17 January 2018

YANGA YALALAMIKA SIMBA KUBEBWA

Klabu ya Yanga kupitia kwa Katibu Mkuu wake wamelalamikia kutokuwepo na usawa kwa Simba na yanga katika matumizi ya viwanja vya Uhuru na ule wa Taifa.

Mkwasa amesema, Yanga kesho inatakiwa kucheza kwenye uwanja wa Uhuru mchezo wake wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga wakati Simba wao watatumia uwanja wa taifa siku ya Alhamisi kwenye mechi yao ya ligi kuu dhidi ya Singida United hivyo amesisitiza kuwepo na usawa kati ya vilabu hivyo juu ya matumizi ya viwanja tajwa.

Kuna wakati bodi ya ligi ilitangaza kuwa, Simba na Yanga zitatakiwa kucheza mechi zao kwenye uwanja wa Azam Complex kupisha shughuli za kiserikali siku ambazo timu hizo zingeutumia uwanja wa Uhuru kwa mechi zao, badala yake yanga ilicheza azam complex mchezo wake dhidi Tanzania Prisons lakini mechi ya Simba ikachezwa kwenye uwanja wa Uhuru.

“Tunatambua kwamba uwanja wa Taifa ulikuwa katika matengenezo na haujatumika kwa muda mrefu lakini kwa sasa unaonekana umekamilika, tulijaribu kuomba tuweze kuutumia lakini tumekosa hiyo fursa na tumepata taarifa kwamba kuna baadhi ya mechi zitachezwa poale lakini sisi mechi yetu ya kesho (Jumatano) itachezwa uwanja wa Uhuru.”

“Tulitegemea tungeanza kucheza pale lakini tunakosa hiyo fursa sasa inatupa shida upande wetu tunaonekana kama hatupewi thamani au umuhimu.”

“Nakumbuka mechi yetu na Prisons yanga ilicheza Jumamosi, Simba wakacheza Jumapili lakini sisi tukacheza kwenye uwanja wa Azam Complex  Simba wakacheza uwanja wa Uhuru kwa hiyo sisi tukakosa hiyo fursa, hii ni mara ya pili inakuwa wenzetu wanaanza kucheza na Singida Alhamisi kwenye uwanja wa taifa sisi kesho tumeambiwa tunacheza uwanja wa Uhuru.”

“Sasa angalieni namna gani hakuna usawa katika mambo kama haya, sisi tunaomba kuwepo na usawa kwa sababu hizi timu zote ni za watanzania wazalendo, kama kuna haki basi itolewe kwa sawa kwa vilabu vyote kuliko kubagua kwamba timu hii inatumia uwanja fulani hii inakosa fursa.”

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search