Wednesday, 31 January 2018

Zitto Kabwe Ataja Viongozi Ambao Atawateua ikitokea Amekuwa Rais wa Tanzania

Image result for zitto kabwe

Mchana wa leo January 30, 2018 kwenye ukurasa wa mtandao wa Twitter wa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika watu ambao atawateua kushika nyadhifa mbalimbali za serikali kama atakuwa Rais wa Tanzania.

Ameandika kuwa atamchagua Mwanaharakati Maria Tsehai Sarungi kuwa Balozi wa Umoja wa Taifa huku Kaimu wake akiwa Mwanzilishi wa Nyama Choma Festival Carol Ndosi.

Amewataja pia Mbunge wa  Arumeru Mashariki Joshua Nassari na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa ACT-Wazalendo Ado Shaibu kuwa atawachagua kuwa Mawaziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ulinzi wa Jamii na Biashara za Umma).

Zitto pia amewataja Mbunge wa Tarime Esther Matiko kuwa Waziri wa TAMISEMI, na Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) mkoa wa Geita Upendo Peneza kushika nafasi ya Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Hata hivyo Zitto ameongeza kuwa ambaye atamteua kuwa Katibu Mkuu Kiongozi hamtaji jina lakini yeye mwenyewe anajijua.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search