Tuesday, 6 February 2018

ALIYEKUTWA NA FEDHA TASLIM BILION 2 AIRPORT AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU AU KULIPA FAINI MIL 100 YEYE KALIPA FAINI NA HIVYO YUKO HURU

Image may contain: 1 person, standing
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imemhuku kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya Shilingi Milioni 100, mwanamke mmoja raia wa Uganda, Winfred Businge, mwenye umri wa miaka 33, kwa kosa la kutembea na pesa taslimu Dola Milioni moja (zaidi ya shilingi Bilioni 2 za kitanzania). Mwanamke huyo alikamatwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere akiwa na kiasi hicho cha pesa kwenye mabegi akisafiri kuelekea China. Hata hivyo Mwanamke huyo amelipa faini ya shilingi milioni 100 na kuepuka kifungo cha miaka mitatu. Baada ya kulipa faini hiyo, mahakama imemrudishia fedha zake (bilioni 2) na kumuachia huru.!

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search