Thursday, 15 February 2018

Aliyekuwa M/Kiti wa UVCCM, Sadifa Hamis ameachiwa huru na kesi ya rushwa dhidi yake kufutwa

Image result for sadifa

Mahakama mkoa Dodoma imemwachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM, Sadifa Hamis baada ya Jamhuri kuwasilisha ombi la kuifuta kesi ya rushwa

Katika shtaka la kwanza alidaiwa Desemba 9,2017 katika makazi yake kwenye Kata ya Mnada mjini Dodoma akiwa mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM aliwahonga wanachama ili wamchague Rashid Mohamed aliyekuwa akiwania nafasi ya makamu mwenyekiti katika uchaguzi mkuu wa umoja huo.

Sadifa katika shtaka la pili alidaiwa katika eneo hilo na siku hiyohiyo, aliwaahidi kuwalipia usafiri wanachama wa umoja huo kuwasafirisha kutoka Dodoma hadi Kagera kama zawadi ili wamchague Rashid Mohamed aliyekuwa akiwania nafasi ya makamu mwenyekiti katika uchaguzi huo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search