Monday, 26 February 2018

ALIYEWAHI KUTANGAZA KUMSHTAKI MH Tundu Lissu ICC AIBUKA TENA

Image may contain: 1 person

Cyprian Musiba, aliyewahi kutangaza kumshtaki Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu katika mahakama ya ICC, leo ameibuka na majina aliyodai kuwa watu hawa ni hatari kwa usalama wa Taifa.Cyprian amemtaja Freeman Mbowe akidai anaongoza kundi la vijana wanaoratibu Uhalifu akiwemo mwanaharakati Yericko Nyerere. Musiba amesema watu hawa wanapaswa kuchunguzwa na kufuatiliwa kila wanalolifanya katika mienendo yao.Katika madai yake amelihusisha shirika la FBI marekani kumtumia Mange Kimambi kuhamasisha vurugu nchini. Majina aliyoyataja akidai ni watu hatari ni: 

1. Freeman Mbowe 2. Mange Kimabi 3.Maria Sarungi 4. Zitto Kabwe 5.Tundu Lissu 6. John Heche 7.John Marwa 8. Evarist Chahali 9. Julius Mtatiro. 

Bila kutoa ushawishi wowote mbele ya wanahabari amedai kuwa anakila kitu kuhusu watu hao aliyodai ni hatari ndani ya Tanzania.Aidha Musiba hakuzungumza madhara ya wazi yalisababishwa na watu hao huku akisisitiza kuwa wamekuwa wakihamasisha vurugu ikiwemo maandamano kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search