Wednesday, 28 February 2018

Asasi za kiraia wafungua kesi Mahakama Kuu kupinga Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu Waandishi wa habari, awali ya yote tunawashukuru na kuwapongeza kwa jinsi mlivyoweza kuitikia wito wetu na kufika kwa wakati ili kutusikiliza ili hatimaye muwe mabalozi wazuri wa kuufikisha huu ujumbe wetu kwa umma wote wa watanzania na dunia nzima kwa ujumla.

Ndugu Waandishi wa habari, Sisi ni Watanzania wapenda haki na usawa katika nchi yetu na tumeamua kutimiza wajibu wetu kwa mujibu wa sheria kufika Mahakamani kutafuta haki dhidi ya masuala mbalimbali ya kisiasa na kiraia.

Ndugu Waandishi wa habari, mtakumbuka kwamba, nchi yetu ipo katika hali isiyo nzuri kidemokrasia, kumekuwepo na matukio kadha wa kadha yanayohatarisha ama yanayozuia ufurahiwajiwa wa haki za kisiasa na kiraia mfano mwenendo mzima wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi kuzuia haki ya mikutano ya kisiasa. Kwa kulitambua hilo, kwa umoja wetu sisi watu 28 wa Kada mbalimbali za kitaaluma ambao ni “Watetezi na Wanaharakati wa Haki za Kisiasa Nchini” tunaopigania haki za Kisiasa Nchini Tanzania kupitia Movement yetu ijulikanayo kama “TUIDAI DEMOKRASIA YETU” tumeona tunazo sababu na tunayoheshima ya kufanya kitu kwa ajili ya taifa letu.

Hivyo basi, tunawafahamisheni kuwa, tayari tumefungua mashauri (2) mawili katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar Es Salaam. Shauri la kwanza lenye No.04/2018 ambalo tayari limefunguliwa Mahakama Kuu linapinga baadhi ya vifungu vya Sheria ya Jeshi la Polisi na katika shauri hili, walalamikaji ni Francis Muhingira Garatwa, Baraka Mwago na Allan Bujo Mwakatumbula na wanatetewa na Wakili Adv.Jebra Kambole.

Aidha, tayari tumefungua shauri lingine (Shauri No.6/2018) Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar Es Salaam ili kupinga baadhi ya vifungu vya Sheria ya Uchaguzi vinavyotumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwaidhinisha Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya kuwa wasimamizi wa Uchaguzi ili hali hawa sio Maafisa wa Tume ya Uchaguzi. Walalamikaji kwenye Shauri hili ni Bob Chacha Wangwe na Mawakili wanaomtetea ni Adv.Fatuma Karume na Adv.Daimu.

Ndugu Waandishiwa habari, lengo letu Kuu ni kuzipigania haki za Kisiasa na Kidemokrasia kwa kuzingatia misingi mikuu ya Kikatiba na Kisheria na kwenye umoja wetu, tupo Wanaharakati, Mawakili na Wanasheria mbalimbali kutoka Kituo cha Haki za Binadamu na Utawala Bora (LHRC) kinachoongozwa na Dr.Hellen Kijo-Bisimba,Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) kinachoongozwa na Mhe.Tundu Lissu na Kituo cha Watetezi wa Haki za Binadamu (THDC) kinachoongozwa na Mr.Onesmo.

Ndugu Waandishi wa habari, washiriki wote katika mapambano ya harakati hizi za kudai haki za msingi kupitia Mahakama zetu ni hawa wafuatao;

1: Adv.Jebra Kambole
2: Adv.Ben Ishabakaki
3: Hon.Sophia Hebron
4: Hon.Baraka Mwago
5: Mr.Raymond Kanegene
6: Adv.Dickson Matata
7: Adv.Pasience Mlowe
8: Hon.Francis Garatwa
9: Hon.Patrick Ole Sosopi
10: Adv.Alex Masaba
11: Hon.Richard Mbalase
12: Mr.Allan Bujo
13: Hon.Bob Chacha Wangwe
14: Dr.Milton Mahanga
15: Mr.Ansbert Ngurumo
16: Adv.Fatuma Karume
17: Adv.John Mallya
18: Adv.Jeremiah Mtobesya
19: Adv.Jonas Mndeme
20: Adv.Harold Sungusia.
21: Mr.Onesmo Olengurumwa
22: Dr.Hellen Kijo-Bisimba
23: Adv.Tito Magoti
24: Adv.John Seka
25: Adv.Fulgence Masawe
26: Adv.Reginald Martin.
27: Adv.Jones Sendodo na
28: Adv.Anna Henga

Ndugu Waandishi wa habari, harakati zetu za mapambano zimeanza miezi (5) mitano iliyopita na yatakuwa endelevu kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

HITIMISHO:

Tunawaomba watanzania watuunge mkono kwenye harakati hizi za mapambano ili kuhakikisha kwamba kwa pamoja tunairejesha nchi yetu kwenye misingi ya utawala wakidemokrasia unaozingatia Katiba na Sheria za Nchi yetu.

Dr.Milton Makongoro Mahanga
Mratibu wa Harakati.

27, February 2018

 FB_IMG_1519756510572.jpg

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search