Saturday, 3 February 2018

ATUPWA JELA KWA KUMUWEKEA MKEWE PILIPILI KWENYE NGUO YAKE YA NDANI

Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Moses Okello amehukumiwa kifungo cha nje na kufanya kazi za jamii kwa siku 40, baada ya kukutwa na hatia ya kumtilia pilipili mke wake kwenye nguo ya ndani 'chupi'.

Mke wa Okello aliiambia mahakama kuwa mume wake huwa anapenda akiwa amevaa nguo hiyo, na siku hiyo alimlazimisha sana kuivaa na kutekeleza, na baada ya muda mfupi alihisi kuwashwa na kuvimba sehemu za siri na kuamua kwenda kumuona daktari, ndipo walipogundua ilikuwa ni pilipili.

“Aliniambia anavutiwa sana na mimi nikiwa nimevaa hiyo nguo akawa ananilazimisha kuivaa, baada ya kuivaa nikaanza kuhisi muwasho sana, nikaenda kumuona daktari na kugundua ilikuwa pilipili”, amesema Mke wa bwana Okello ambaye jina lake limehifadhiwa.

Moses alikiri kufanya tukio hilo kwa mkewe, na kusema kwamba ulikuwa ni utani ambao amezoea kufanyiana na mke wake huyo kipenzi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search