Thursday, 1 February 2018

AUAWA KWA KUCHUNWA NGOZI NA WATU WASIOJULIKANA NA BAADHI YA VIUNGO VYAKE KUTOLEWA

Inasikitisha!.... Auawa na Kuchunwa Ngozi na Kutolewa Viungo vya Mwili Wake na Watu Wasiojulikana
Mzee mmoja aliyetambulia kwa majina ya Tuntinala Kunyepa (75) mkazi wa Kijiji cha Ihanda Wilayani Mbozi Mkoani Songwe, amekutwa akiwa ameuawa na kuchunwa ngozi na kisha kutolewa baadhi ya viungo vya mwili wake na watu wasiojulikana .


Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Songwe, Yusuph Sarungi, amesema, tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo na kwamba, hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hiilo huku mauaji hayo yakihusishwa na imani za kishirikina ambapo uchunguzi na msako mkali unaendelea kuwabaini waliohusika .

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search