Tuesday, 6 February 2018

CUF yamtaka Diwani wao kuacha kuandamana na mgombea wa ChademaKatibu wa CUF Ally Mkandu amemtaka Diwani wa kata ya mzimuni Ally Kondo kuacha kuongozana na mgombea wa Chadema Salum Mwalimu.

Amesema kwamba diwani huo asipoacha kuongozana na mgombea huyo chama kitamchukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kutumia katiba kumvua uanachama.

Mkurugenzi wa Habari na uenezi Abduli Kambaya amewaambia wakazi wa mzimuni kwamba mwaka 2015 CUF ilipata ushindi kwa kufanya kazi kubwa kwenye kata ya mzimuni.

‘’Leo anajitokeza mtu anawashawishi mumchague mgombea mwingine inauma sana’’amesema Kambaya

Naye mgombea Rajabu Salum amesema kwamba ‘’Mimi nilikuwa meneja kampeni wa mgombea wa huyu aliyehamia CCM( Maulid Mtulia) hivyo mimi nilikuwa mwalimu wake’’

Amesema mgombea huyo sasa ameanza kutumia sera za Cuf kwenye majukwaa.

‘’CCM na Chadema wameahidi kunipa kura kwa kuwa wagombea wao hawakushiriki kwenye kura za maoni ‘’amesema Salum

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search