Tuesday, 6 February 2018

Dr. Slaa(Balozi): Siendi kutekeleza Sera ya CCM bali Sera ya Taifa. Aongelea sakata zima la Lowassa kuingizwa CHADEMASlaa anasema gari lake limeshawahi kukamatwa na cocaine tani tano mwaka 1991 na lilikaa polisi miaka 8 ila uzuri alilikodisha kwa kampuni hivyo yeye hakuusishwa. Baada ya hapo aliingia kwenye siasa na anaelezea nafasi alizoshika CHADEMA.

Anasema baada ya hapo watu wanasema ameondoka kwenye siasa, anasema Serena Hotel alisema anaachana na siasa za vyama vingi na active politics, na akaahidi kutokuwa mwanachama wa chama cha siasa na amejiuzulu siasa za vyama.

Amesema, Serena alisema mtu akihitaji jambo la kupigiwa kelele lenye maslahi atalipigia kelele.

Anasema yeye hakusepa wala kufukuzwa kanisa katoliki bali alifata taratibu za kutoka na alipata decree ya kutoka mwaka 1998 ndio maana yeye hana tatizo na kanisa katoliki. Ndio maana hata lilipokuja suala la ndoa, anasema ndoa haifungwi na padri bali ndoa inafungwa na wahusika wawili, padri ni ofisa.

Amesema February 2016 alifunga ndoa ya validation kwenye kanisa katoliki, anasema yeye amekuja nchini kwa sababu ni mwenyekiti wa CCBRT na sio mambo ya ubalozi. Amesema nchini kuna mabadiliko mengi na wao CCBRT wameguswa, ilitakiwa kujiandikisha upya na waliandikiwa kuwa wanaweza kufutiwa usajili, sheria iliyotungwa mwaka 2002 na kufanyiwa marekebisho 2015. Hivyo kilichomleta ni mchakato wa kuhamisha usajili wa shirika.

Slaa anasema Canada ni nchi ambayo ni kama haina mwenyewe, miaka 500 iliyopita watu wengi walihamia, wao wanaona popote ulipotoka, ukifika Canada wewe ni mcanada. Anasema Canada, kazi ni maisha na sio msemo kama Tanzania na ndio maana ya maendeleo. Anatolea mfano watu wanavyofika ofisini na kufikia kusoma magazeti karibu saa nzima au kunywa chai.

Anasema nchi ni tajiri na watu pia matajiri na ni kwa sababu wanafanya kazi, pia huduma zote ziko standard.

Slaa: Balozi siendi kutekeleza sera ya CCM, naenda kutekeleza sera ya taifa. Mambo yakishaingia bungeni na kupitishwa hayawi tena ya CCM, yanakuwa ya taifa. Anatolea mfano Karatu walivyotekeleza sera ya Taifa kwa namna ya CHADEMA kwa sababu walikuwa na madiwani theluthi mbili.

Slaa anatolea mfano walivyomsomea Mkapa sera ya zahanati kila kijiji Karatu na yeye alivyofika Arusha akaifanya sera ya taifa kwa zahati kila kijiji nchi nzima. Kuhusu kauli ya Mnyeti kuhusu watendaji wasiounga mkono serikali, amesema itakuwa ni makosa kwani analazimisha.

Kuhusu kadi za CHADEMA na CCM, anasema hakurudisha kadi ya CCM na sheria inasema uanachama unajulikana kwa kadi lakini pia kuonekana kwenye jukwaa la chama kingine unakuwa sio mwanachama. CHADEMA alisema ameondoka lakini kadi ni kumbukumbu yake na ameilipia hivyo ni haki yake.

Amesema mwelekeo wa siasa nchini haumfurahishi, anasema baada ya Uhuru kulikuwa na vyama vingi, baadae vikaanza kufa vyenyewe kwa sababu vilikatisha tamaa wananchi na baadae vikaondoka kisheria.

Anasema anasikitika kwa sababu ameshiriki kujenga upinzani nchini na haoni chama chenye sera zilizonyooka. Mikakati ya utekelezaji kwa serikali iliyoko madarakani duniani kote ni kipindi cha kutoa ahadi na sera sera mbadala na hakuna mtu anaesema wameiba au wamenyang'anya kwani sera ikitoka hadharani ni za nchi nzima.

Kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, amesema kama binadamu, hakuna anayependa binadamu mwenzake aumizwe lakini matukio ya kuumiza yanatokea nchini kwa watu wengi sana na yeye sio chombo cha dola kunyoosha mkono kwa mtu, amesema mwananci wa kawaida anaweza kuwa mtu anamuhisia lakini yeye ni msomi, kama ana taarifa anaenda kuripoti.

Anasema alipotaja list of shame, alipata maadui na alitishwa lakini wakati huo alikuwa na mtandao mkubwa wa chama wa kumlinda lakini leo hana na aliondoka kwenye chama hana mtandao na waliokuwa wanamlinda walimgeuka kuwa maadui zake hivyo akahamia Canada kwani inajulikana duniani kwa human rights record na ni nchi isiyokuwa na mwenyewe.

Slaa anasema yeye amekuwa padri hivyo hana kisasi na mtu na siasa haiwezi kumfanya awe na kisasi na mtu, kama padri wa kikatoliki anakumbuka biblia inasema nini, anajua theolojia hivyo hawezi kuwa na kisasi na mtu. Amesema mawasiliano ya kawaida na Gwajima yapo ila hayawezi kuwa kama kipindi kile.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search