Tuesday, 6 February 2018

FA KUCHUNGUZA ISHARA YA TROY DEENEY YA KUONESHA KIDOLE CHA KATIChama cha soka cha England FA kuchunguza kitendo cha mshambuliaji wa Watford Troy Deeney alipoonyesha kidole cha kati baada ya kufunga penalti dhidi ya Chelsea wakiwapa kichapo cha goli 4 - 1 jana.

Lilikuwa ni goli la kwanza la mechi na lililoipa faida ya kuongoza kipindi cha kwanza, huku akijiandaa kupiga mkwaju huo wa penalti, mashabiki wa Chelsea walionekana kumdhihaki na baada ya kuingia kambani alionekana kuonyesha kidole cha kati kwa mashabiki hao.

Baada ya mechi kumalizika, Ripota na mtangazaji wa michezo wa Skysports mwanadada Michelle Owen kupitia ukurasa wake wa Twita ameandika kwamba aliongea na Deeney na mchezaji huyo amesema kwamba hiyo ni njia yake ya kuonyesha kwamba bado yupo Watford baada ya taarifa za yeye kuondoka klabuni hapo wiki kadhaa zilizopita.

Deeney amekuwa na historia mbaya siku za karibuni, akifungiwa mechi tatu Oktoba mwaka jana baada ya kukamata uso wa Joe Allen wa Stoke City na Disemba kufungiwa mechi nne baada ya rafu mbaya aliyomchezea Collin Quaner wa Huddersfield.

Dele Alli akiichezea timu ya taifa England alifanya kitendo kama hicho mwaka jana wakati wa mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Slovakia, tofauti ni kwamba hakuwaelekezea mashabiki. Alifungiwa mechi moja na kupigwa faini ya paundi 3800.

Troy anaweza kufungiwa mpaka mechi 4 kama adhabu ya kitendo alichokifanya ikiwa FA bado inapitia video hiyo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search