Thursday, 8 February 2018

GEITA: Watumishi wa wawili wa Serikali wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za rushwa

takukuru+pic.png
Watumishi wanne wa Serikali katika mikoa ya Mwanza na Geita wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita, imewaburuta mahakamani watumishi wawili wa kitengo cha maabara katika Kituo cha Afya cha Uyovu kwa tuhuma za kupokea rushwa.

Waliofikishwa mahakamani mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Bukombe, Gabriel Kurwijila ni Sylivester Kalekwa na Abbas Nyamizi.

Mwendesha mashtaka wa TAKUKURU, Husna Kiboko ameieleza Mahakama kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Februari 2 mwaka kwa kupokea Sh25,000 kutoka kwa ndugu wa mgonjwa kama kishawishi cha kumpatia vifaa vya kutolea damu, kinyume na kifungu cha 15(1) na kifungu cha pili cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Husna amesema washtakiwa hao pia walitenda kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume na kifungu cha 302 cha kanuni ya adhabu.

Washtakiwa walikana mashtaka hayo huku mshtakiwa wa kwanza, Kalekwa akiachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh4 milioni pamoja na wadhamini wawili.

Mshtakiwa wa pili, Nyamizi alipelekwa mahabusu hadi Februari 20 shauri hilo litakapotajwa tena baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.


Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search