Tuesday, 27 February 2018

HII NDIO KAULI YA ZITTO BAADA YA HUKUMU YA SUGU


Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kuwataka Wabunge wa vyama vya upinzani wasimame mbele ili waweze kuhesabiwa ili wapate kujitambua wamebakia wangapi.

Zitto amebainisha hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kutolewa kwa hukumu ya Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga kwenda jela miezi mitano kutokana na kukutwa na hatia ya kutoa maneno ya fedheha dhidi ya Rais Magufuli.

"Nimeona mashtaka ya Sugu yaliyopelekea kuhukumiwa kwenda jela miezi 5. Wabunge wote wa vyama vya upinzani kwa namna moja ama nyingine tunasema haya kila wakati kwenye mikutano yetu. Kuna haja ya kufanya jambo ambalo dola itaamua kutusweka jela wote au kutorudia walichofanya kwa Sugu", amesema Zitto.


Kwa upande mwingine, Zitto amedai anawasiliana na wenzake ili waweze kupata 'united Democratic Front'

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search