Friday, 2 February 2018

HIZI HAPA NI KAULI MBALIMBALI ZA WANASIASA NA WATU MASHUHURI KWENYE INSTAGRAM PAGE ZAO KUFUATIA KIFO CHA MZEE KINGUNGE


FREEMAN MBOWE
Baba yetu Mzee Kingunge Ngombare Mwiru ametutoka, ni huzuni kubwa kwa mara nyingine na pigo kubwa katika Taifa letu, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.Ni wakati mwingine wa majonzi tena na wakati mgumu kuliko wakati mwingine wowote katika maisha ya mwanadamu pale anapotwaliwa mmoja wetu.

Tunaahidi kuyaendeleza yale mazuri uliyokuwa ukiyaamini, tutayapigania bila woga, ulikuwa na msimamo, hukuyumbishwa, uliyasema unayoyaamini kwamba ndio yanayotakiwa kwa wakati tuliopo, najua ulitamani uone mabadiliko ya kweli ndio maana uliungana na upinzani na ukaongoza mapambano kuelekea mabadiliko ya kweli, hakika tutakukumbuka daima, umetuacha safarini lakini si mbali tutafika.

Tunakuombea kwa Mungu Mzee Kingunge Ngombare Mwiru, upumzike kwa amani baba yetu, umekuwa kiongozi imara na shupavu katika Taifa la Tanzania milele tutakukumbuka kwa misimamo yako.

Mbele yetu,nyuma yako, Bwana alitoa,Bwana ametwa jina lake lihimidiwe,Amina.

MANGE KIMAMBI
R.I.P shujaaa wa taifa, Mzee Kingunge afariki alfajiri ya leo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
.
.
Mzee Kingunge atakumbukwa na historia ya nchi kama kiongozi mwenye msimamo mkali wa kisiasa. Kingunge ni mfano wa kuigwa na vijana wa taifa letu, mpaka mauti yanamkuta Kingunge aligoma kurudi kwenye chama alichosaidia kukianzisha sababu aliamini hakikuaa na manufaaa tena kwa mtanzania na aliweza kumtamkia Rais Magufuli usoni kwake kuwa ameitapika CCM...... Watanzania wengine ilibidi wafate mfano wa huyu mzeee, CCM sio baba yenu wala mama yenu kama waliokianzisha hiko chama walitoka na mpaka siku zao za mwisho za maisha walikataa kurudi chamani, wewe ndo inajua CCM kushinda kina Kingunge?e We ndio unaipenda CCM kuliko kina Kingunge??Eti unaenda kumuunga mkono Rais, 😏
.
.
Kingunge ametuachia somo moja kubwa sana, Taifa kwanza, chama baadae. R.I.P Shujaa wa ukombozi!!!!

JULIUS MTATIRO
Mzee aliyekuwa anaamini TAIFA KWANZA! Mzee Kingunge ni mfano halisi wa wazee wachache wenye uwezo wa kusimamia wanayoyaamini bila kuhofia madhara ya misimamo yao. Mzee huyu anawakumbusha vijana kuwa YAPO MAISHA mazuri sana hata unapoamua kutoyumbishwa, tusemeje sasa? Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Pole sana kwa familia, kumpoteza baba na mama kwa nyakati zinazokaribiana ni jambo gumu na lisilovumilika, lakini tutafanya nini? Sisi ni binadamu tu! R.I.P Mzee Ngombale!

HUSSEIN BASHE
Rest In Peace Mzee Kingunge Ngombale Mwiru

Mwaka 2007 kwa mara ya kwanza nili kutana na wewe Comrade Ngombale uliniita pale dodoma baada ya mkutano mkuu ukanipa Moyo juu ya Tukio la kisiasa ambalo lilinitokea pale dodoma.Nakumbuka uliniambia Comrade usivunjike Moyo falsafa ya mapambano ya kifikra na kisiasa yanamaumivu wewe kijana kuwa jasiri usikate Tamaa

Toka wakati huo tulijenga mahusiano ya Karibu umenijenga Mimi na vijana wengi sana ndani ya UVCCM

Mwaka 2008 uliniita nyumbani kwako tukakaa kwenye viti vya Plastiki vyeupe pale uwani kwako ulinihoji Comrade kwanini unataka kuwa Kiongozi wa UVCCM ukiwa kamanda nilijieleza swali la Mwisho uliniuliza Unamfahamu Rajab Diwani? Ukanipa Historia yake Kwangu Comrade na vijana wengi kina Martine Shigela kina Kapenjama kina Ridhwani kina Beno kina Nchimbi kina Nape na wengine wengi kwa njia tofauti walipita mikononi mwako

Mwaka 2015 uliniita ulipoamua kujiondoa CCM uliniambia 
Comrade umeamua kuwa Mbunge kutumikia watu Simamia Unachoamini simamia Haki unaenda dodoma kuapishwa watu Wako wana Matarajio Tazama maslahi ya Nchi yako watu Wako na Chama chako usiyumbishwe usiunge mkono dhulma tulikunywa chai ya Rangi ya mchai chai .

Comrade umeenda mbele ya Haki ukiwa Huna deni umeshiriki kujenga Tanu na CCM umejenga vijana wengi umeshiriki kwa Nguvu zako zote kusimamia Unachoamini wewe kuwa ni Haki toka wakati wa Mwalim JK Nyerere ulifukuzwa ukuu wa Mkoa kwa kusimamia Haki na kile unachokiamini sisi vijana tuliokulia ndani ya UVCCM na CCM hatuwezi kusahau mchango Wako ndani ya chama na Taifa hili nakumbuka ulikua ktk harakati za ku rekodi na kuandika Historia ya UVCCM na mchango Wako na wanaharakati wengine ktk ukombozi wa Taifa letu na mataifa ya kusini

Comrade ur gone physically but u will always remain in our memories 
R I P

HENRY KILEWO

R.I.P MZEE KINGUNGE... Mzee wetu ametuachia Somo kubwa sana Sisi Vijana Wataifa hili, Somo lenyewe ni Msimamo thabiti usiyotiliwa Shaka.
.
Mzee alikuwa Kitandani lakini hakusita wala kutetereka kuusema Msimamo wake japokuwa alikuwa hoi Kitandani, Ingalikuwa ni Mtu asiyekuwa na Msimamo Thabiti angeropoka, ila alijijua yeye ni nani na kutuonyesha Vijana ya Kwamba enzi zao za Ujana hawakuwa watu wa kuyumbishwa au Kushangilia tu kwakuwa amekuja Mkubwa.
.
Hili ni Deni kwetu sote vijana tuachane na kutanguliza Matumbo yetu mbele na Ubinafsi usiyokuwa na Maana, Tubaki kwenye Misingi Imara ya kupigania Haki na Demokrasia yakweli ili tuache alama isiyotiliwa shaka na Vizazi vijavyo kama ambavyo Mzee KINGUNGE alivyofanya.
.
Huruka ya kujipendekeza pendekeza inatudhalilisha Vijana, Tunaonekana Takataka za Kisiasa yaani Watu wasiyojielewa ndani ya Taifa Lao.
.
Nenda kapumzike mahala salama Mzee wetu KINGUNGE, Umetimiza wajibu wako na Kulitumikia Taifa lako bila kutiliwa shaka yeyote Ile.
.
Poleni sana Familia ya Mzee KINGUNGE, Watoto,Ndugu Jamaa na Marafiki na Wapiganaji Wote.
.
Tumeondokewa na Jabali la Kisiasa lililozeeka na Maono na Msimamo Imara,Alikataa kujikomba..Vijana tunadeni la Kulipa, Acha Kuuza Utu wako.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search