Tuesday, 27 February 2018

KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA APATA AJALI

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo amepata ajali katika eneo la Mdori mkoani Manyara baada ya gari alilokuwa akilitumia kupasuka gurudumu 'tairi' ya nyuma na kupoteza uelekeo.


Hayo yamethibitishwa na mlinzi wa Kamanda Mkumbo (Bodyguard) wakati alivyokuwa anazungumza na mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu ya RPC na kusema ni Kamanda Mkumbo amepata ajali hiyo ambapo ndani ya gari aliyokuwa akiitumia walikua watu watatu akiwemo msaidizi wake pamoja na dereva.

Kamanda Mkumbo amepelekwa katika hospitali ya Mount Meru mkoani humo baada ya kupata maumivu aliyokuwa nayo ya kichwa kutokana na ajali hiyo aliyoipata.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search