Saturday, 3 February 2018

KATAMBI ATAJA SABABU ZA KUHAMIA CCM

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi aliyehamia CCM Novemba, 2017 ametoa sababu sita za kukihama chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 2, 2018 jijini Dar es Salaam, Katambi amesema ameamua kueleza hayo baada ya kujipa muda wa kutafakari kwa kina.

Amesema sababu ya kwanza ni vyama vya upinzani ikiwamo Chadema kushindwa kujipambanua kama taasisi, badala yake kuwa kama cha mtu binafsi.

Katambi amesema sababu nyingine ni ukosefu wa maamuzi shirikishi, ukiukwaji wa katiba na misingi ya demokrasia, kutokuwa na mawasiliano na umoja na kukosa maadili kwa viongozi.

"Hali hii ya ukosefu wa maadili inasababisha matumizi mabaya ya mali za chama na sababu ya mwisho ni chama kukosa ajenda," amesema Katambi.

Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search