Tuesday, 6 February 2018

LISSU ATEMBELEWA NA VIONGOZI WA UMOJA WA ULAYA

DVRdQCIW0AAgVxz.jpg ​

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mbunge wa Singida Kaskazini, Mhe. Tundu Lissu , leo ametembelewa na maofisa watatu kutoka Makao Makuu ya Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa ajili ya kumjulia hali na kufanya nae mazungumzo juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Tanzania.

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya (EU) umeongozwa na Mkuu wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki katika Wizara ya Nje ya EU, Bw. Patrick Simonnet.

Kutoka kushoto ni Bw. Patrick Simonnet; Mke wa Mhe Lissu, Alicia,Mkuu wa Dawati la Tanzania katika EU, Bi Marta Szilagyi,Mh. Lissu; Bi. Hortensia May Lyatuu na Bi. Vania,ambaye ni afisa wa Ubalozi wa EU Tanzania anayeshughulikia masuala ya utawala bora na haki za binadamu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search