Wednesday, 21 February 2018

MADIWANI WAWILI WA CHADEMA HUKO ARUSHA MJINI WAHAMIA CCM

Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Musa Matoroka amewapokea madiwani Prosper Msofe na Obed Meng’oriki wa CHADEMA ambao walitangaza kujivua uanachama jana.
Wawili hao walitoa tangazo jana kwa waandishi wa habari la kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM kwa madai kuwa wanataka kuunga mkono jitihada za uongozi wa Rais John Magufuli.
Matoroka ametoa ujumbe kwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuwa wamejiandaa kuchukua jimbo hilo hivyo aanze kutafuta kazi nyingine.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search