Monday, 5 February 2018

Mahakama ya Rufaa yafutilia mbali kifungu cha Sheria kinachosotesha watu rumande, Mtobesya ambwaga mwanasheria mkuu

MAHAKAMA YA RUFAA YASISITIZA KIFUNGU CHA 148(4) CPA KINAVUNJA IBARA 13(6)(a) YA KATIBA YA NCHI
Image result for mahakama

Kwa mujibu wa nakala ya hukumu hiyo inaonyesha imesainiwa na Msajili wa Mahakama ya Rufani, John Kahyoza, Januari 31 Mwaka huu, inasema jopo la Majaji wa Tano walioketi Dar Es Salaam.

Jaji Bernad Luanda, Kipenka Mussa, Mmilla, Mugasha na Jacob Mwambegele kwa Kauli Moja walitoa hukumu hiyo ya ya kutupilia rufaa hiyo Na.65/2016 iliyokuwa imekatwa mahakamani hapo na Mwomba Rufani ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mjibu Rufani ( Mtobesya ).

Jaji Kipenka alisema jopo hilo baada ya kupitia Sababu nne za Mwomba rufaa kukata rufaa ambazo miongoni mwa Sababu hizo Kuwa Mahakama Kuu ilikosea Kusema Kifungu hicho kinamnyima fursa mshitakiwa kupinga hati hiyo ya DPP ya Kuzuia dhamana na kwamba Mahakama Hiyo ilikosea kisheria kukubali kutolea uamuzi shauri ambalo Mwombaji alikosea kunukuu Ibara ya Katiba hoja ambazo Jaji Mussa alisema hazina mashiko.

" Mahakama ya rufaa imetupilia Mbali kwa gharama rufaa iliyokatwa Mbele yetu na Mwanasheria Mkuu wa serikali iliyokuwa ikiomba Mahakama hii itengue uamuzi ya Mahakama Kuu uliokuwa umetamka kuwa Kifungu 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwa sababu ni kweli Kifungo hicho kinakwenda kinyume na Ibara ya 13 (6)(a) ya Katiba ya nchi.

"Na Mahakama hii ya Rufani nayo inakubaliana na hukumu ya Mahakama Kuu Kuwa Kifungu hicho cha 148(4) Sheria hiyo ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinafunja matakwa ya Ibara hiyo ya Katiba hivyo uamuzi wa Mahakama Kuu ulikuwa sahihi na Mahakama hii imekataa kutengua uamuzi ule hivyo utabaki kama ulivyo na Mwanasheria Mkuu wa serikali alipe gharama za Kesi kwa Mjibu Rufani( Mutobesya).

Ibara ya 13(6) (a) ya Katiba ya nchi inasomeka hivi ;

"Wakati Haki na wajibu kwa mtu yeyote inapoitajika kufanyiwa maamuzi na Mahakama au Chombo kingine chochote kinachohusika, basi mtu Huyo Atakuwa na Haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia Haki ya kukata Rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya Mahakama au Chombo hicho kingine kinachohusika".

Disemba 22 Mwaka 2015, Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam Katika Kesi ya Kikatiba Na 29 /2015 ,Shabani Lila ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa sasa,Kihiyo na Ruhangisa ambaye alistaafu Ujaji wa kwa Hiari mwaka 2017 ,ambapo jopo hilo lilikubaliana na hoja za malalamikaji Mtobesya Kuwa Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ,kina kwenda kinyume na Ibara ya hiyo ya Katiba ya nchi.

Mwaka 2016, Mwanasheria Mkuu wa serikali alikata rufaa Mahakama ya Rufani nchini, kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu akiomba utenguliwe uamuzi huo kwasababu nne ambazo miongoni mwa Sababu hizo ni kwamba Mahakama ilikosea Kusema hati ya Kufunga dhamana ya mshitakiwa inayowasilishwa mahakamani na DPP inammnyima mshitakiwa Haki ya kuipinga hati hiyo ya DPP Katika Chombo kingine.

Desemba 22 Mwaka 2015 , Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam Katika Kesi ya Kikatiba Na 29 /2015 ,iliyofunguliwa na Mtobesya dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Shabani Lila ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa sasa,Kijiyo na Ruhangisa ambaye alistaafu Ujaji wa kwa Hiari ambapo jopo lilikubaliana na hoja za malalamikaji Mtobesya Kuwa Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ,kina kwenda kinyume na Ibara ya 13 (6)(b) ya Katiba ya nchi.

Kwa Mujibu wa hati yake ya Madai ilioambatanishwa na kiapo Chake Juni 30 mwaka 2015 ,Mutobesya alidai Kuwa Ibara 26 ( 2) ya Katiba ya nchi inasomeka kama ifuatavyo;

"Kila mtu Ana Haki , kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria , kuchukua Hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na Sheria za nchi".

Na Kuwa Kifungu cha 4 na 5 Cha Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Binadamu(BRADEA)

Hivyo alitumia Kifungu na Ibara hizo za Katiba kwenda Kufungua Kesi Mahakama Kuu ili kuiomba Mahakama Kuu itamke Kuwa Kifungu cha 148(4) cha Sheria hiyo kinakwenda kinyume na Ibara 13(b)(a) ya Katiba ya nchi na kwamba Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya nchi inampa Haki ya kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi.

Itakumbukwa Kuwa Kifungu hicho cha 148(4) cha Sheria hicho ,ndicho kilichotumika Kumfungia dhamana Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu ,Sheikh Issa Ponda.Kifungu hicho pia kulitumika Kumfungia dhamana kwa Mara ya pili Mkoani Morogoro ambapo alikuwa na Kesi ya uchochezi.

Pia Kifungu hicho ndio kilitumika kumuweka ndani Mh.Lema Mbunge wa Arushaa na kimetumika na DPP Kuzuia dhamana ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (SUGU) ambaye anasota gerezani wakati kosa alishitakiwa nalo lina dhamana.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search