Wednesday, 28 February 2018

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU BAADA YA KUONEKANA HANA KESI YA KUJIBU

Image result for mahakama
Mtuhumiwa Adolph Msafiri aliyekuwa akishtakiwa kwa kosa la kutoa lugha ya kuudhi dhidi ya Jeshi la Polisi ameachiwa huru na mahakama ya Mwanzo huko mkoani Mtwara baada ya kuonekana hana kesi ya kujibu. Mtuhumiwa huyo alikamatwa kwa kuweka ktk ukurasa wake wa Facebook, picha ya Askari Polisi wakishambulia raia siku ya maandamano ya Chadema February 16, mwaka huu na kuandika "KUNA TOFAUTI KATI YA POLISI NA TAKATAKA"
_
Hakimu Lawrence Nyoni aliyesikiliza kesi hiyo amesema anamuachia huru Adolph kwa sababu mashtaka dhidi yake hayana msingi wowote kisheria.

Awali Mtuhumiwa alipokua akijitetea alimhoji askari wa upelelezi aliyekuwa mahakamani hapo kuwa "wewe ni polisi?" Akajibu "ndio" akamuiliza tena "unafanana na takataka?" Akajibu "hapana", mtuhumiwa akasema "kwahiyo unakubaliana na mimi kwamba kuna tofauti kati ya polisi na takataka sio?". Askari huyo hakujibu.

Adolph ni mwanafunzi wa sheria, Chuo Kikuu Huria kampasi ya Dar es Salaam.!

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search