Monday, 26 February 2018

MAITI YATUPWA DUKANI

Wakazi wa Voi katika Kaunti ya Taita Taveta walipigwa na bumbuwazi na hali ya sintofahau, baada ya ndugu kuutupa mwili wa marehemu Amos Mwabanga, kwenye duka la mfanya bishara mkubwa wa eneo hilo.

Tukio hilo ambalo limetokea hivi karibuni, limekuja baada ya familia ya merehemu kuhisi kuwa mfanya biashara huyo ndiye anahusika na kifo cha ndugu yao, ambaye alikuwa mfanyakazi wake, baada ya kumtuhumu kumuibia.

Familia hiyo imeendelea kuelezea kwmaba mfanyabishara mkubwa wa eneo hilo amemtuhumu ndugu yao kuua kondoo wake na kumuibia mbuzi, sambamba na wafanyakazi wenzake wawili, kitendo ambacho kilichomfanya aende kwa mganga na ndipo ndugu yao alipokutwa na umauti.

“Baada ya kuchukua dawa waliyopewa na mganga na kunywa, walianza kupatwa na maumivu makali na kufariki baada ya muda mfupi”, alisikika mmoja wa wanandugu akielezea tukio hilo.

Waombolezaji ambao walifika eneo hilo walimtaka mfanyabiashara huyo atoke nje lakini hawakufanikiwa kumpata, na polisi kulazimika kuingilia kati kwa kuwatawanya kwa mabomu ya machozi, na kisha kuutoa mwili na kuurudisha mochwari baada ya familia kuaacha hapo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search