Wednesday, 28 February 2018

Mambo Matano aliyoyakubali Tido Mhando baada ya kusomewa maelezo

Leo February 28, 2018 Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando amesomewa maelezo ya awali (Ph) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo amekana kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Milioni 800.

tido-4-660x400.jpg 

Awali kabla ya kusomewa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa, Tido alikumbushwa mashtaka yanayomkabili na Wakili wa Serikali Dismas Mganyizi.

Katika maelezo hayo, Tido alikubali wasifu wake binafsi na kwamba aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC mwaka 2006 hadi 2010.

Pia alikubali kuwa alikuwa msimamizi katika shughuli za TBC lakini sio kwa shughuli zote.

Pia alikubali kutoa maelezo katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) lakini hakukiri na kuwa alifikishwa mahakamani January 26,2018.

Kwa upande wa mashtaka yanayomkabili, Tido aliyakana yote ikiwemo kuisababishia serikali hasara kupitia TBC ya zaidi ya Shilingi Milioni 800.

Baada ya kukana tuhuma hizo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi March 28,2018 kwa ajili ya mashahidi wa upande wa mashtaka kuanza kusikilizwa.

Tido anakabiliwa na mashtaka matano ikiwemo kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Shilingi Milioni 887.1.

Inadaiwa kuwa June 16, 2008 akiwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido ambaye alikuwa mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

Pia anadaiwa kuwa kati ya June 16 na November 16, 2008 akiwa UAE, Tido aliisababishia TBC hasara ya Sh887,122,219.19.

Chanzo: Millard Ayo

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search