Friday, 2 February 2018

Mapenzi Yamtesa Mwanaume Mwenye Maumbile Marefu Duniani "Nimeachika Mara 10 Lakini Sikati Tamaa"

Mwanaume Mwenye Maumbile Marefu Duniani Ahangaikia Mwanamke wa Kuishi Naye "Nimeachika Mara 10 Lakini Sikati Tamaa"
Wakati kukiwa na kasumba ya wanawake kuwachekwa kama sio kuwadharau wanaume wenye maumbile madogo hapa Afrika, hii ni tofauti kabisa na  Roberto Esquivel Cabrera mwanaume pekee duniani anayekadiriwa kuwa na maumbile marefu zaidi duniani ambaye anahangaika hadi leo kupata mwanamke wa kuishi wa kuishi naye.

Roberto Esquivel Cabrera (54) raia wa Mexico amesema amekuwa akipata tabu kuchagua wanawake kwani amedai kipindi akiwa sekondari miaka 30 iliyopita wanawake wengi walikuwa wanampenda lakini kadri umri ulivyozidi kukua maumbile yake yalikuwa yanaongezeka na kuanza kumnyima raha kwani alianza kukimbiwa na wanawake.

Kwenye mahojiano yake na mtandao wa IFL Science, Cabrera amesema amefanikiwa kupata mtoto mmoja tu kwenye maisha yake na mke wake wa kwanza ambaye naye alimkimbia kutokana na ukubwa wa maumbile yake.

Cabrera amesema mpaka kufikia sasa amefanikiwa kuishi na wanawake 10 lakini wote wamemuacha sababu kubwa ni kukosa furaha ya tendo la ndoa.

“Nilipokuwa kijana wa miaka 20+ nilikuwa najiona mwanaume haswa kwani hata sikuwa naogopa wanawake na nilipendwa kweli lakini kadri muda ulivyozidi kwenda nikawa nahisi maumivu kwenye sehemu zangu za siri kitu ambacho kilianza kuniumiza kisaikolojia nikaanza kuwa mpweke kwani kila mwanamke niliyetaka kwenda naye faragha alinikimbia,“amesema Cabrera.Cabrera amesema ameenda hospitali mara kadhaa akihitaji dawa za kupunguza maumbile yake lakini alichoshauriwa ni kufanyiwa upasuaji mdogo kiytu ambacho hakuafikiana nacho.

“Kuna watalaamu walikuja baada ya kuandikwa na vyombo vya habari wakitaka kunifanyia upasuaji nilikataa napenda niwe hivi hivi najua, kuachika na wanawake kumi hakunifanyi nikose amani najua Mungu ataniletea mwenzangu mwenye maumbile yanayoendana na yangu bado sikati tamaa,“amefunga Cabrera.

Cabrera amesema hata kama akiona amechelewa kupata mwenza nchini Mexico atasafiri hadi Marekani ambako amesema atapata wanawake wenye maumbile makubwa kwani huwa anawaona kwenye picha chafu (Video za X) na anaamini atapata mke.

“Mimi nimeshakuwa mtu maarufu kutokana na maumbile yangu siwezi kuyapunguza nitaenda Marekani kule kuna wanawake wengi wenye maumbile makubwa huwa nawaona mitandaoni, siwezi kupunguza kamwe,“amesema Cabrera kwenye mahojiano yake na gazeti la The Sun la Uingereza.

Kwa upande mwingine Madaktari wamesema kuwa Cabrera kama angetahiriwa akiwa mdogo huenda asingelipatwa na tatizo hilo kwani linachangiwa na ongezeko la homoni.

Maumbile ya Cabrera yanakadiriwa kuwa na urefu wa nchi 18.9 hadi 20 pale yanapokuwa yamesimama na kumfanya kuwa mwanaume wa kwanza mwenye maumbile marefu zaidi duniani aliyerekodiwa.

Hata hivyo bado Cabrera hajaingizwa kwenye kitabu cha maarufu cha kumbukumbu cha (Guinness World Records). Tazama mahojiano yake hapa chini aliyowahi kufanya kipindi cha nyuma (Video by Barcroft TV)

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search