Monday, 5 February 2018

Mbowe ashangazwa na marufuku ya kupiga salamu ya vyama vingine


Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe amesema ameshangazwa kupigwa marufuku kutoa salamu ya vyama vingine katika mikutano ya uchaguzi inayoendelea kufanyika huku akidai sheria hiyo haipo bali ni sheria ya hofu.

Mbowe ametoa kauli hiyo ikiwa yupo katika muendelezo wa kumuombea ridhaa mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia (CHADEMA), Salum Mwalimu kuwa Mbunge wa eneo hilo katika siku zijazo za usoni ambapo kwa sasa zimebakia takribani siku 12 tu uchaguzi mdogo kufanyika.

"Juzi kimeitishwa kikao ambacho kina mashitaka dhidi ya CHADEMA na mengine ni wanaopenda haki katika taifa hili. Kikao kile kikaamua kwamba kwenye mikutano iwe ni marufuku kusalimiana kwa salamu za chama kingine", amesema Mbowe.

Pamoja na hayo, Mbowe ameendelea kufafanua baadhi ya mambo kwa kusema "nikashangaa kidogo, tukija kwenye mkutano hapa Kinondoni hatuji kuzungumza na wanachadema peke yao maana uwanja huu  wapo wanawacuf, wanaccm sasa iweje uniambie Mbowe usitoe salamu ya CUF katika mkutano. Hiyo sheria katika uchaguzi haipo ni sheria ya hofu kwa hiyo mimi natambua uwanjani hapa wapo wanacuf na nina haki ya kuwasalimia wote".

Kwa upande mwingine, Mbowe amesema kusalimia ni hiari yake hivyo hawezi kupangiwa kufanya hivyo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search