Wednesday, 28 February 2018

Mbowe: Hukumu ya Sugu ilipangwa hotelini na RC Makalla. TISS wanaratibu mikakati ya kutubambikia CHADEMA kesi
Mwenyekiti Mbowe

=> Mauwaji yanayotokea na yanayoendelea kutoka Serikali inapotosha kwa kusema wanaofanya mauwaji hayo hawajulikani ni dhahiri mauwaji hayo Serikali inajua wanaofanya ukali huu.

=> Jana wakati tupo kwenye mazishi ya Godfrey J. Lweno Morogoro wananchi walikitaka Chama kitoe kauli ya kulipiza kisasi. Sasa tunaanza kuona jinsi gani wananchi wameshaanza kuchoka, Chadema tunalitakia mema Taifa hili ingawa watawala hawaoni umuhimu.

=> Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Amosi Amosi Makala anahusika kuratibu kesi ya Sugu (Joseph Mbilinyi). Wamekua wakifanya figisu ili Mbunge wetu afungwe

=> Hukumu ya Mbunge wa Mbeya Mjini ni dhahiri inaonekana kuwa watawala wanaendelea kuratibu mateso kwa viongozi wa Upinzani, na tuliofahamu mapema juu ya kilichoratibiwa na tulimkataa hakini lakini bado Hakimu aliendelea kusimamia kesi hiyo na dhamira yake mbaya.

=> Hukumu ya Sugu ilifahamika na ilipangwa Hotelini, wote tulifahamu, polisi walichukuliwa wilayani kwenda Mbeya mjini na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amosi Makala anajua hilo.

=> Jeshi la Polisi imempiga Akwilina risasi na kupoteza uhai wake lakini baadae wanaanza kugeuza kibao kwamba CHADEMA nao walikuwa na vikosi vyao.

=> Hivi sasa hivi tunavyoongea Jeshi la Polisi linawashikilia vijana waliopigwa risasi na hawajawapeleka Mahakani wala kuwapa huduma.

=> Roho ya ubinadamu haipo kwa watawala wetu. Unampiga mtu risasi ya moto halafu unamuweka ndani siku 13 bila kumpa matibabu stahiki. Humpeleki mahakamani lakini bado unamnyima dhamana.

=> Unatumiaje risasi za moto kuzuia waandamanaji tena ambao wanafanya maandamano ya amani. Kweli polisi unachukua bunduki unapiga risasi za moto kuzuia maandamano ya amani. Hii sio Tanzania tunayaoifahamu hii ni Tanzania ya Bwana Magufuli

=> Tunajua Jeshi la Polisi linawanyima dhamana wahanga waliopigwa risasi ili kuficha maovu ya Jeshi la Polisi na wanajua wakiwaachia waandishi mtawaona na mtawahoji hii sio Tanzania tunayoijua.

=> Hakuna wakati wowote wa Uchaguzi uliokua mbaya kama kipindi hiki cha marudio ya Uchaguzi. Basi angalau wangetuibia kura kwa akili kama ilivyokuwa zamani. Lakini Uchaguzi wa hivi karibuni, aisee tumetambua kuwa Mkurugenzi wa Tume anapewa maagizo na viongozi wake wa juu

=> Hizi chaguzi zitaendelea kuzaa maumivu kwasababu wenzetu wanafanya fujo za kila aina kwenye chaguzi na wanalindwa na Dolla kama hatua stahiki hazitachukuliwa tutaliingiza Taifa hili kwenye machafuko.
=> CCM kama wanataka kurudisha uhalali wao wa uongozi waseme na wananchi watawaelewa na sio kutumia bunduki kukatisha uhai wa watu. Halafu tumeshaanza kuzoea kuuwawa, hili jambo si zuri maana tunakoelekea ni kutaka kuua upinzani.

=> Jambo hili sio la kushabikia ni hatari kwa taifa letu lazima tuchukue hatua.. Haya mambo hayakuwepo mwanzoni

=> Kuna mtu anaitwa Musiba anasema CHADEMA imepeleka zaidi ya vijana 500 kwenda kusoma Ujerumani, huyu ni mpumbavu tu. Anataja watu kama kama akina @YerickoNyerere_ sisi hatujasomesha watu

=> Usalama wa Taifa wanaratibu mikakati ya kutubambikia kesi wana CHADEMA. Sasa sisi tumejipanga kutokana na huo mkakati. Tunamwambia Mh. Rais Magufuli, sisi tuko tayari kwa lolote, tunapigania demokrasia.

=> Mkoa wa Morogoro unaongoza kwa kuwabambikizia kesi viongozi wetu wa CHADEMA. Lakini hata kwa mauaji, Mkoa huo unaongoza maana kuna historia ya watu wetu wa CHADEMA kuuwawa mkoani Morogoro

=> CHADEMA sio chama cha kigaidi. Serikali itambue kwamba hiki ni chama makini.

=> Watambue kwamba wataua vyama vya siasa lakini hawataua mioyo ya wanachama. Utaua CHADEMA au CUF lakini sio wanachama.

=> Tunamwambia Rais na wanaotekeleza mkakati huu kuwa hatutarudi nyuma, watawaumiza wengi lakini hawatakata tamaa.

=> Nitaongoza viongozi wenzangu sita kwenda kuripoti kama Jeshi la Polisi lilivyotutaka, ingawa tunajua yanayopangwa lakini hatutaogopa na wala kurudi nyuma.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search