Tuesday, 20 February 2018

Mbowe, Mnyika na viongozi wengine wa Chadema waachiwa

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewaachia kwa dhamana viongozi waandamizi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA. walioitikia wito uliotolewa na jeshi la polisi.
[​IMG]
Vingozi wa Chadema wakiripoti kituoni hapo

Waliripoti kituoni hapo kufuatia wito uliotolewa na jeshi la polisi jana kutokana na kifo cha mwanafunzi, Akwilina aliyefariki kwa kupigwa risasi na jeshi la polisi.

Kwa mujibu wa ITV, Viongozi hao walioripoti leo ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh.Freeman Mbowe,Katibu Mkuu CHADEMA Dokta Vicent Mashinji,Naibu Katibu Mkuu Bara John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu,Mbunge wa Tarime mji Mh.Estar Matiko,Mbunge wa Tarime vijini John Heche na Mbunge Kawe Mh.Halima Mdee

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search