Tuesday, 6 February 2018

Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari afikishwa Mahakamani.


nas.jpg
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru akisubiri kusomewa shitaka linalomkabili.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumanne Februari 6,2018, Nasari amesema jana alikwenda Kituo cha Polisi Usa River kufuatilia silaha yake iliyochukuliwa na askari wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014.

Nassari amesema alipofika polisi alielezwa kuwa ana kesi ya kumshambulia mtendaji kosa analodaiwa kutenda mwaka 2014 .

Sheki Mfinanga ambaye ni wakili wa Nassari amesema hajui mteja wake anakabiliwa na shtaka gani.

"Jana walisema alishambulia lakini hatujui leo anashitakiwa kwa kosa gani ndiyo tunasubiri," amesema.

Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search