Tuesday, 6 February 2018

MSIBA WA KINGUNGE WAKUTANISHA VIONGOZI MBALIMBALI,MAZISHI YAFANYIKA

Rais Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Marais wastaafu wa Tanzania na viongozi mbalimbali,wakiwa katika shughuli maalum ya kumpumzisha aliyekuwa Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru,makaburi ya kinondoni Dar es salaam
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiweka udongo kwenye kaburi la muasisi wa Taifa na mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru ambaye anazikwa leo katika makaburi ya KInondoni Jijini Dar es salaamMarais wastaafu,Dr.Jakaya Mrisho Kikwete,Benjamin William Mkapa na Ali Hassan Mwinyi wakiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mwanasiasa nguli na mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru katika makaburi ya kinondoni Jijini Dar es Salaam
Viongozi wa Serikali walio madarakani na wastaafu wakiongozwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wamejumuika na waombolezaji wengine kuaga mwili wa mwanasiasa mkongwe nchini, marehemu Kingunge Ngombale Mwiru.


Shughuli ya kuaga mwili wa Kingunge imefanyika leo Jumatatu Februari 5,2018 katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.


Viongozi wengine walioaga mwili wa Kingunge ni marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa aliyeambatana na mkewe Anna; Makamu wa Rais mstaafu, Dk Mohamed Gharib Bilal; mawaziri wakuu wastaafu Dk Salim Ahmed Salim, Frederick Sumaye, Edward Lowassa na mkewe Regina; na Jaji mstaafu Joseph Warioba.


Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula na mtangulizi wake Pius Msekwa; Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Othman Chande; Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.


Pia, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole; Mama Maria Nyerere; Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye; na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search