Monday, 5 February 2018

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mteule, Dkt. Adelardus Kilangi ameapishwa rasmi Bungeni


Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi Aapishwa Bungeni
Dodoma. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Adelardus Kilangi amekula kiapo cha uaminifu bungeni, kukabidhiwa vitendea kazi na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

Dk Kilangi ameapa leo Februari 5, 2018 kabla ya kuanza kwa kikao cha tano cha mkutano wa 11 wa Bunge, mjini Dodoma.

Mara baada ya kuapa, Dk Tulia alimkabidhi AG vitendea kazi hivyo. Februari Mosi, 2018 Rais Magufuli alimteua Dk Kilangi kuwa AG mpya na Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Pia, alimtea aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na naibu wake, Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu.

Februari 3, 2018 wateule hao waliapishwa na Rais Magufuli Ikulu, Dar es Salaam na kueleza mikakati yao katika majukumu yao mapya.

Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search