Wednesday, 21 February 2018

Mwandishi wa Mwananchi akamatwa kwa kumpiga picha Makonda eneo la kutangazia matokeo


Mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi, Ibrahimu Yamola jana alishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kumpiga picha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Yamola alimpiga picha Makonda aliyekuwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi wakati wa kutangaza matokeo ya ubunge jimbo la Kinondoni katika kituo cha Biafra, Kinondoni jiji Dar es Salaam.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu, Yamola alisema, alikamatwa wakati akipiga picha viongozi hao waliokuwa kwenye eneo hilo la kutangazia matokeo ya ubunge ambapo chama cha Mapinduzi kupitia mgombea wake, Maulid Mtulia kiliibuka mshindi.
Yamola alisema, wakati akipiga picha hizo aliitwa na Makonda na kumhoji kwanini anampiga picha hizo.
“Nimempiga picha ya kwanza mpaka ya tatu, Makonda akaniita akaniuliza kwanini nampiga picha, nikamjibu kama hairuhusiwi kupigwa picha aniwie radhi, akaniambia lete simu yako akafuta zile picha, alisema na kuongeza
Baada ya kufuta picha akamwita Kamanda wa kanda maalim ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na kunikabidhi kwake, wakanipeleka kwenye gari lao hadi kituo cha Polisi Oysterbay”
[​IMG]

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search