Saturday, 3 February 2018

PIC: Kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) imejiendesha kwa hasara kwa miaka mitatu mfululizo


Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), imetaja mashirika matatu yanayojiendesha kihasara ikiwa ni pamoja na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ambayo imejiendesha kwa hasara kwa miaka mitatu mfululizo.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli zake katika mwaka wa 2017, mwenyekiti wa kamati hiyo, Albert Ntabaliba alisema kamati yake imebaini kuwa taasisi nyingi zimekuwa zikijiendesha kwa hasara kwa sababu mbalimbali ikiwamo matumizi makubwa kuliko mapato.

Alitoa mfano wa ATCL ambayo matumizi yake yamekuwa yakiongezeka kwa kiasi kikubwa na hivyo kuifanya kampuni kujiendesha kwa hasara.

“Katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2014/15 hadi 2016/17 matumizi yaliongezeka kwa kiwango cha juu ikilinganishwa na mapato yaliyokusanywa na kusababisha kampuni kupata hasara kwa miaka yote mitatu mfululizo,” alisema.

Alifafanua kuwa katika mwaka 2014/15 hasara ilikuwa Sh94.3 bilioni, mwaka 2015/16 ilipata hasara ya Sh109.3 bilioni na mwaka 2016/17 ilipata Sh113.8 bilioni na kwamba hali hairidhishi na kama itaendelea kama ilivyo uhai wa kampuni hiyo upo shakani.

Pia, alisema kamati imebaini uwapo wa matumizi makubwa katika Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kuliko mapato, hali iliyosababisha kuwapo kwa nakisi ya Sh397.9 milioni kwa mwaka 2013/14.

Alisema nakisi ya mamlaka hiyo kwa mwaka 2014/15 ilikuwa ni Sh614.6 milioni na mwaka 2015/16, Sh838.2milioni.

“Uchambuzi umebaini kuwa ongezeko hilo kubwa la matumizi limechangiwa na ongezeko la matumizi mengineyo, mishahara na gharama za utawala,”alisema.

Hata hivyo, alisema gharama za uwekezaji (gharama za maonyesho na kutangaza bidhaa na utafiti) zimepungua kutoka asilimia 32.5 mwaka 2011/12 hadi asilimia 16.8 mwaka 2015/16 ambazo zilipaswa kupanda kwa lengo la kukuza kipato cha taasisi hii.

Ntabaliba alisema kamati yake imebaini kuwa Shirika la Elimu Kibaha limekuwa likipata nakisi kwa miaka mitatu mfululizo ya wastani wa Sh1.2 bilioni kwa mwaka.

Alisema mwaka 2012/13, nakisi imeongezeka kutoka Sh482 milioni hadi Sh3.2 bilioni mwaka 2014/15 na kwamba katika miaka miwili ya mwisho, naksi imekuwa ikipungua hadi kufikia Sh955 milioni mwaka 2016/17.

Akichangia taarifa za kamati, Mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka alihoji kuwa utafiti gani uliofanyika kabla ya kununua ndege mpya wakati ATCL imeendelea kupata hasara kwa miaka mitatu mfululizo.

“Hali si nzuri kwa kampuni hiyo lakini Serikali imeendelea kununua ndege mpya. Wakurugenzi na bodi inaonyesha wameshindwa kufanya kazi na Serikali isipochukua hatua kampuni hii inakwenda kufa,” alisema.

Vibali vya sukari

Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, imeishauri Serikali iandae utaratibu rafiki wa uingizaji na utoaji sukari ya viwandani bandarini na kurejesha kwa wakati asilimia 15 ya kodi ya sukari ya viwandani.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Suleimain Sadick alishauri wafanyabiashara wawe waaminifu kwa Serikali katika kutoa taarifa za uzalishaji na kodi.

Kamati ya Bunge ya Bajeti imeishauri Serikali kuhakikisha kuwa ukopaji na ulipaji wa deni la Taifa hauathiri ugharamiaji wa bajeti ya Serikali kwa kila mwaka wa fedha.

Akisoma utekelezaji wa shughuli za kamati hiyo, mwenyekiti wa kamati hiyo, Hawa Ghasia aliitaka Serikali kukamilisha kazi ya tathmini ya nchi kukopa na kulipa madeni.

“Aidha Serikali iendelee kufanya majadiliano na taasisi, nchi na Benki ya Dunia wanaoidai nchi ili kupata masharti nafuu katika ulipaji wa Deni la Taifa kama walivyofanya Kenya na Malawi,” alisema.

Ghasia alisema kwa mujibu wa Serikali, deni la Taifa ni himilivu na kwamba fedha nyingi zinazokopwa ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Serikali haijakamilisha tathimini ya uwezo wa nchi kukopa na kulipa madeni ili kuongeza uwezo zaidi wa Serikali kukopa kwenye vyanzo nafuu,” alisema.

Kuhusu sekta ya mabenki, Ghasia alisema hivi karibuni benki zimekumbwa na msukosuko hasa baada ya benki tatu kuwekwa chini ya uangalizi na tano kufungiwa kati ya 15.

Alisema kwa sababu moja ya tatizo kubwa lililozikumba benki hizo ni usimamizi mbovu wa bodi za mabenki hayo, kamati hiyo inaishauri Serikali kupitia Benki Kuu kuanzisha kitengo maalumu chini ya idara ya usimamizi wa mabenki.

Chanzo: Mwananchi

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), imekuwa ikipata hasara sana. Mara ya Mwisho Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, bwana Ladislaus Matindi alisema ATCL imepunguza hasara kutoka Sh bilioni 20 hadi kufi kia Sh bilioni 3 kwa mwaka. Sababu kubwa ya hasara ilielezwa ni ufutaji wa safari,

Pamoja kwamba ATCL ni Shirika kongwe la Umma, lakini bado inamiliki ndege mbili aina ya Bombardier Q400 Zilizonunuliwa na Serikali ya awammu ya Tano.


Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), imetaja mashirika matatu yanayojiendesha kihasara ikiwa ni pamoja na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ambayo imejiendesha kwa hasara kwa miaka mitatu mfululizo.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli zake katika mwaka wa 2017, mwenyekiti wa kamati hiyo, Albert Ntabaliba alisema kamati yake imebaini kuwa taasisi nyingi zimekuwa zikijiendesha kwa hasara kwa sababu mbalimbali ikiwamo matumizi makubwa kuliko mapato.

Alitoa mfano wa ATCL ambayo matumizi yake yamekuwa yakiongezeka kwa kiasi kikubwa na hivyo kuifanya kampuni kujiendesha kwa hasara.

“Katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2014/15 hadi 2016/17 matumizi yaliongezeka kwa kiwango cha juu ikilinganishwa na mapato yaliyokusanywa na kusababisha kampuni kupata hasara kwa miaka yote mitatu mfululizo,” alisema.

[​IMG]
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Mhe. Albert Obama (Mb) akizungumza wakati Kamati yake ilipokwenda kukagua mradi wa Ujenzi wa Nyumba katika eneo la Kawe na Morroco Jijini Dar es Salaam.

Nashauri Serikali iipe ATCL uwezo wa kusimamia vitega uchumi Vyake ili kujikwamua kwenye mkwamo huu.

Wataalam wa ndege wastaafu nchini walishawahi kuishauri Serikali ya awamu ya Tano kuhakikisha inarudisha vitega uchumi muhimu vya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ili iweze kujiendesha kwa faida.

Walipendekeza mambo mengi ambayo hayafanyiwi kazi. Baadhi ya mambo hayo ni;

wataalam hao pia walishauri kuundwa kwa kitengo maalum cha ATCL ambacho kitasimamia shughuli zote kwa kugawanywa katika maeneo ya usimamizi wa mizigo, abiria, mifumo ya kompyuta, mabasi ya kuwachukua abiria na mizigo, ulinzi na mengineyo.

i). Serikali kuunda na kukiwezesha ipasavyo kitengo cha uhandisi cha ATCL ambacho kinaweza kuwa chanzo cha kuzalisha mapato kwa kutengeneza ndege za kigeni pale zinapopata matatizo huku kikihakikishia uimara wa ndege za Serikali kwa gharama nafuu.

ii). Walipendekeza Serikali kuangalia namna ya kuipa ATCL uwezo wa kuuza mafuta ya ndege T3. “Huduma ya kuuza mafuta ya ndege T3 sio lazima apewe PUMA au Oil Com kwa sababu biashara hii ina maslahi sana basi serikali inaweza kuipa ATCL ikishirikiana na kampuni nyingine yenye uzoefu,” alisema.

Waliongeza kuwa kuiwezesha ATCL kutaisaidia Kampuni hiyo kujiendesha yenyewe na kuhimili ushindani wa soko ikiwa ni pamoja kuwalipa mishahara na stahiki zote wafanyakazi wake bila kutegemea kiasi chochote kutoka Wizara ya Fedha (Hazina).

iii). Walimuomba Waziri wa Mawasiliano na uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amshauri Rais Magufuli kutumia mamlaka yake kurudisha vitega uchumi ambavyo ATCL iliporwa na Mafisadi waliokuwa katika Serikali za awamu ya pili, ya tatu na ya nne ambao hawakujali maslahi ya shirika la ndege la Taifa ATC/ATCL na badala yake wakayapa upendeleo mkubwa baadhi ya mashirika ya ndege ya mataifa mengine ambayo hayanufaishi nchi,” alisisitiza.

iv). Walitahadharisha kuwa watakuwepo watu wengi wasiopenda maendeleo ya kampuni hiyo watakaopinga ushauri wao wakitaka ATCL ijikite katika biashara ya kurusha ndege tu. “Tunaiomba serikali ya awamu ya tano ihakikishe kuwa shirika la ndege la taifa ATCL linarudishiwa mamlaka ya kumiliki ground handling za airport zote za tanzania bara na hasa viwanja vikubwa kama Julius Nyerere International Airport Dsm, Kilimanjaro International Air Port, Mwanza Air Port, Kigoma Air Port, Songwe Air Port, Mtwara Air Port, Dodoma Air Port n.k." alisema Mhandisi mstaafu wa shirika la ndege la Taifa ATC, J. Mwandimo

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search