Wednesday, 7 February 2018

Prof. Kabudi: Rais wa Jamhuri ana mamlaka ya kuwaagiza mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi (Zanzibar)


Waziri wa katiba na sheria profesa Palamagamba Kabudi amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana mamlaka yote ya kutoa maagizo kwa mawaziri ambao wapo ndani ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri Kabudi ameliambia bunge kuwa kikatiba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mkuu wa nchi hivyo Katiba inamruhusu kufanya hivyo.

Amesema jamii inapaswa kutambua kuwa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar pia ni mjumbe wa baraza la mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Profesa Kabudi ametoa ufafanuzi leo bungeni baada ya wizara yake kuulizwa bungeni kufuatia Rais Dr.John Magufuli kuonekana akitoa maagizo kwa waziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na yule Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo: ITV

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search