Tuesday, 6 February 2018

Serikali: Asilimia 1 ya Watanzania ni wagonjwa wa akili. Yasisitiza kutokuwepo kwa uhaba wa dawa muhimu

Image result for bungeni
Suala hilo limesemwa leo Februari 6, 2018 Bungeni na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akijibu swali kutoka kwa Mbunge wa Morogoro Kusini (CCM), Prosper Mbena aliyetaka kujua ni kwa nini Serikali haina utaratibu wa kuchukua wagonjwa wa akili wanaozunguka mitaani.

Aliuliza;“Je serikali inafahamu idadi ya wagonjwa wa akili waliopo barabarani na mitaani kwenye wilaya zote nchini ambao wanahitaji huduma ya matibabu, inatoa maelekezo gani kwa waganga wakuu wa wilaya kuhusu kuwahudumia wagonjwa hao,”

Naibu waziri alijibu na amesema kuwa;

“Wagonjwa wa akili ni asilimia moja tu ya watanzania wote, hivyo kati ya Watanzania milioni 50, wagonjwa wa akili ni watanzania laki 5”

Pia amesema kuwa ni ngumu kwa wizara ya afya kuwa na idadi kamili maana si wagonjwa wote wa akili wapo hospitalini.

“Si wagonjwa wote wa akili wako hospitali, wengi wao wanarandaranda mitaani hivyo basi si rahisi sana kwa Wizara ya Afya kufanya utafiti na kujua idadi kamili ya wagonjwa wa akili.”

Hata hivyo, amekiri kuwa jamii imekuwa ikiwanyanyasa, kuwabagua na kuwatenga wagonjwa wa akili na kusababisha waranderande mitaani.

Aidha, Naibu waziri amezungumzia suala la matibabu ya wazee hospitalini na matunzo yao kwa Ujumla. Naibu waziri amesema kuwa jukumu la kwanza la matunzo ya wazee ni familia. Pia aasisitiza kuwa matibabu ya wazee ni bure

“Jukumu la kwanza la kutunza wazee ni la familia, serikali inakuja mwishoni. Ninatoa wito kwa jamii nzima ya Watanzania kulisimamia hilo,”

“Matibabu ya wazee wasiojiweza yanatolewa bure…na ninaomba ieleweke wazi kwamba serikali haina uhaba wa dawa muhimu kwani bajeti ya dawa imeongezwa”

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search