Friday, 9 February 2018

Serikali: Uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma umekamilika. Yatalipwa mwezi wa pili pamoja na mshahara

Image result
Waziri wa fedha na Mipango Dr.Philip Mpango amesema Serikali italipa madeni inayodaiwa ya Zaidi ya shilingi bilioni 43 ambazo imezihakiki na kuona kuwa ni madeni halali ambayo wanadaiwa kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2017 na watumishi wa umma wakiwemo Walimu.

Waziri Mpango amesema fedha hizo zitalipwa kwa mkupuo na watumishi watakaolipwa madai hayo ni elfu ishirini na saba mia tatu themanini na tisa na yatalipwa sambamba na mishahara ya mwezi huu wa pili.

Waziri Mpango amesema awali watumishi elfu themanini na mbili mia moja kumi na moja waliwasilisha madai ya shilingi bilioni mia moja na ishirini na saba ,milioni mia sita na tano laki moja na ishirini na nane,mia nane na sabini na mbili na senti themanini na moja.

Kwa mujibu wa Waziri Mpango,Serikaki imeokoa shilingi bilioni themanini na nne na milioni mia mbili na laki mbili kufuatia uhakiki huo ambazo ni sawa na asilimia 66 ya madai yote yaliyokuwa yamewasilishwa awali.

Malipo ya madai haya ambayo mengine yana zaidi ya miaka 10, majina ya walipwaji yatatangazwa kwenye magazeti kuanzia kesho tarehe 10 Februari

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search