Tuesday, 6 February 2018

Sheikh wa Mkoa Mussa Alhad, atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheriaSheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salim hivi sasa anazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusiana na kuhusishwa na kampeni zinazoendelea katika Jimbo la Kinondoni.

Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Mussa Alhad ameelezea picha inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye kufanya kampeni ambayo yumo yeye na pembeni kuna mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akila chakula pamoja na wenzake wa CCM. Amesema picha ilipigwa akiwa kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail, amesema yeye ni kiongozi na mtu yeyote anaweza kupiga picha na yeye.

Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mbalimbali kwenye Instagram na kusema pia alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali na Rais John Magufuli.

Sheikh Alhad amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kudai Mange anautumia ulimi na mikono yake vibaya kudhulumu watu(Heshima zao).

Alhad amesisitiza huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi au mkono wake kwa sababu amejihalalishia mwenyewe maangamizi kwa mkono wake. Amesema atamshtaki kwenye mahakama ya Mbinguni.

Kingunge.jpg ​

Amesema kuna watu walimpa rai asimjibu kwani atamtukana sana na kudai wao wanataka aendelee kutukana na hatasikia sauti yake baada ya leo ikimjibu na yeye andelee kutukana.

Alhad amesema hawezi kujiingiza kwenye kampeni ya kuipigia debe CCM, amesema CCM ina kawaida ya kualika viongozi wa dini na chama chochote kinaweza kumualika kwenye jambo lake. Amesema ajabu, picha zake ndio zinaanikwa lakini za viongozi wengine hazianikwi.

Katika hatua nyingine, Sheikh ameiambia NEC kuhusu JamiiForums ambao wameandika kwamba sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam: Hivi mnajua kama anafanya kampeni Kinondoni! Alhad amesema watachukua hatua za kisheria ili wathibitishe sheikh wa mkoa wapi amefanya kampeni, kwa kuhudhuria kwenye maziko au sababu ya picha!.

Hivyo kuhusu JamiiForums, wataona namna gani ya kushughulika nao kisheria na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine, wajiingiza katika jambo hilo kichwa kichwa bila kulijua ili kuvunja heshma zao.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search