Thursday, 8 February 2018

TANZIA: Mwanasiasa maarufu, Richard Tambwe Hizza afariki Dunia

tambwe1.jpg
Mwanachama wa CHADEMA, Richard Tambwe hiza amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake. Mwili wake umepelekwa Hospitali ya Temeke Dar Es Salaam asubuhi hii. Hadi jana saa tano usiku alikuwa kwenye Kikao cha CHADEMA.

Marehemu Tambwe Hizza amefariki akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu na amefariki akiwa ni mmoja wa waratibu wa kampeni za chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) katika jimbo la Kinindoni

Hizza anafahamika sana kwa siasa zake akiwa CUF, Baadae alihamia CCM na kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa CCM na 2015 aliamua kuondoka CCM na kuhamia CHADEMA. Mwaka 2014 alisema angegombania Urais kupitia cha mapinduzi kwani uwezo, akili, elimu na afya ya kumuwezesha kuwa Rais wa tano wa Tanzania.

Jana alishiriki kampeni za kumnadi Salum Mwalimu Tandale mapema jioni kabla ya Vikao vya chama.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search