Wednesday, 21 February 2018

Tunduma: Mbunge Frank Mwakajoka akamatwa kwa amri ya mkuu wa wilaya

[​IMG]

Mbunge wa CHADEMA katika jimbo la Tunduma, mkoani Mbeya, Frank Mwakajoka amekamatwa na kuwekwa ndani kwa saa 48 kwa amri ya mkuu wa wilaya.

Mwakajoka ameswekwa rumande baada ya kuwapiga picha na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii, madiwani watatu wa Chama hicho waliojiengua na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wanadaiwa kupigwa picha na Mwakajoka, ni Ayob Mlimba ambaye alikuwa diwani wa Kata ya (mwaka kati), Simon Mbukwa (Kaloleni), na Amos Nzunda (Mpemba).

Taarifa zinasema, tukio hilo lilitokea wakati madiwani hao walipoitwa na serikali kuhudhuria kikao cha bajeti cha Halmashauri ya Mji mdogo wa Tunduma, leo Jumatano.

"Hawa watatu wa nyuma ndio waliokuwa madiwani wetu wa CHADEMA na ambao wamejiuzulu nafasi zao. Lakini leo wameitwa kwenye kikao cha bajeti ya Mji, huku wakiwa wamehama chama na kujiuzulu nafasi zao za udiwani", ameeleza Mwakajoka katika moja ya ujumbe wake kwa wabunge wenzake.

Muda mfupi baadaye, mbunge huyo anaandika " Na sasa nawekwa chini ya ulinzi na pia nakaa ndani kwa saa 48 kwa amri ya (DC mkuu wa wilaya)", aliandika mbunge huyo Mwakajoka.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search