Sunday, 4 February 2018

Uchambuzi wa Mtatiro J kuhusu ATCL kujiendesha kwa hasara

Image result for mtatiro
Mwenyekiti wa Kamati bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PIC) Mhe. Albert Ntabaliba ameeleza kuwa kwa miaka miwili mfululizo tangu serikali inunue ndege mbili aina ya Bombardier, zimeleta hasara ya Shilingi Bilioni 109.3 + Bilioni 113.8 = Bilioni 223.1. 

Yaani, mwaka wa fedha 2015/2016 taifa limepata hasara ya Shilingi Bilioni 109.3 na mwaka wa fedha 2016/2017 (uliomalizika Septemba 2017) tumepata hasara ya shilingi bilioni 113.8.

Kama fedha hizi zilizopotea (Bilioni 223.1) zingeliwekezwa kwenye barabara zetu, miundombinu yetu, maisha yetu na uchumi wetu kwa ujumla zingelileta tija kubwa kwa taifa. 

Fedha hizi zingeliweza kununua matrekta makubwa 7436 na kila kata ya Tanzania ingelipewa matrekata mawili ambayo yangelilima maelfu ya ekari za mazao kwa siku na kulizalishia taifa matrilioni ya fedha.

Fedha hizo zilizopotea, kama zingelitumika kutoa mikopo ya elimu ya juu ya kiwango cha shilingi milioni 5 kwa mwanafunzi mmoja, zingeliweza kusaidia wanafunzi 55,775 kwa mwaka mzima au wanafunzi 18, 591 kwa miaka mitatu mfululizo ya masomo.

Fedha hizo kama zingelitumiwa kutoa mikopo ya shilingi Milioni moja moja kwa vijana wajasiramali wadogo, zingeliweza kusaidia jumla ya vijana 223,100 nchi nzima, vijana 7,436 katika kila mkoa, vijana 1,203 katika kila wilaya, Vijana 74 katika kila kata na vijana 18 katika kila kijiji. 

Kama vijana hao wangelipewa kwanza elimu ya ujasirimali na baadaye wakarudisha pesa hizo, kila mwaka wa fedha vijana wapya kwa idadi hiyo hiyo nchi nzima wangenufaika na fedha hizo.

Taifa letu na uongozi wa sasa hautaki kusikiliza tahadhari zinazotolewa na wataalamu na watu wanaoona masuala ya uchumi wa nchi yakiwa hayako sawa. Serikali inataka kusifiwa tu, kwamba inajenga reli, barabara, inanunua ndege n.k. Serikali imeshajitoa kwenye utaratibu wa kujiendesha kwa uwazi. Serikali haitaki ushauri wa mtu. 

Serikali yetu haiambiliki! "Call it any name"ndiyo maana baada ya miaka mitano tutakuwa na hali mbaya sana kwa hasara hizi kubwa tunazopata na utawala huu ukishaondoka madarakani tutakuja kugundua matrilioni ya fedha yaaliibiwa au kupotezwa kupitia kwenye miradi ambayo haikukaguliwa na vyombo vinavyohusika wala haikuidhinishwa na bunge.

#Mtatiro J

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search