Sunday, 4 February 2018

WAFANYAKAZI WAANZA KUKATWA MISHAHARA KUFADHILI UCHAGUZI WA 2020

Wafanyakazi wa umma nchini Burundi wameanza kukatwa asilimia 10 ya mishahara yao kwaajili ya kufadhili uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwaka 2020.
Katika kipindi cha miaka miwili ijayo, raia wote wa Burundi walio na zaidi ya umri wa kupiga kura wa miaka kumi na minane na zaidi, ni sharti wachangie katika hazina hiyo ya kitaifa.
Serikali ya Burundi imesema imechukua uamuzi huo ili kuziba pengo lililosababishwa na uamuzi wa wafadhili wa kuzuia misaada tangu mzozo wa mwaka 2015 wakati rais Pierre Nkurunziza alipowania muhula wa tatu.
Hata hivyo serikali imekariri kuwa hazina hiyo ya uchaguzi ni wazo la raia wa Burundi wenyewe, pendekezo ambalo limepingwa na wakuu wa vyama vya wafanyakazi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search