Monday, 5 February 2018

WASTARA ATOBOA SIRI YA KILICHOMTOA KWA MUME WAKE

Msanii wa filamu bongo ambaye hivi karibuni amekuwa akipokea michango kutoka kwa watu mbali mbali kwa ajili ya matibabu, ameweka wazi moja ya sababu iliyofanya ndoa yake na kigogo wa CCM Sadifa Khamis kuvunjika baada ya muda mfupi.

Akizungumza na mwandishi wa eatv Wastara amesema mume wake huyo alionesha kutojali matatizo yake na badala yake kuweka pesa mbele, baada ya kudai risiti za matibabu aliyoenda kutibiwa India, kwa hela za michango ya watu mbali mbali, ili arudishiwe na bunge na ziingie mfukoni mwake.

Wastara amesema kitendo cha Sadifa kudai risiti hakikukifurahia, kwani pesa aliyokwenda nayo haikutoka mfukoni mwake, bali zilitoka kwa watu mbali mali wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, Msanii Alikiba, rafiki yake Sadifa na wengineo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search