Tuesday, 20 February 2018

Waziri Ndalichako, Anna Makakala wa Uhamiaji na TCU watinga chuo kikuu cha Kampala. Wafanyakazi 30 wakamatwa

Asubuhi hii waziri wa elimu, Prof Ndalichako akiambatana na maafisa kutoka idara ya Uhamiaji wameibukia chuo kikuu cha Kampala(KIU) na kuangalia vibali vya wageni wanaofanya kazi katika chuo hiko.nda.jpgnda3.jpg
Waziri Ndalichako amepokelewa na wanafunzi huku Uongozi wa shule ukikosekana.

Ashangazwa na wanachuo wa mwaka wa kwanza licha ya kufanyiwa utambulisho wa mazingira na uongozi wadaiwa kutofahamu viongozi wakuu wa chuo.

Kwa sasa waziri Ndalichako ameenda maabara na anahoji vitu kadhaa ikiwemo kujaribu mashine zinazofanya kazi kwenye maabara pia anawauliza maswali kadhaa wanafunzi wa chuo hiko kwa ahadi ya zawadi ikiwemo jina la mkuu wa chuo chao.


UPDATES

Saa chache baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako kufanya ziara Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), wafanyakazi 30 wa chuo hicho wamekamatwa wakituhumiwa kufanya kazi nchini bila vibali.

Katika ziara hiyo iliyofanyika leo Februari 20, 2018 Profesa Ndalichako ameambatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Anna Makakala, mkuu wa Ithibati na Udhibiti Ubora wa Vyuo, Dk Valerian Damian na maofisa mbalimbali kutoka uhamiaji na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Profesa Ndalichako amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwamo walimu wa chuo hicho kuajiriwa sehemu zaidi ya moja na kuishi nchini bila vibali.

Kufuatia upekuzi mkali, wafanyakazi 30 wamekamatwa na Uhamiaji wakituhumiwa kutokuwa na vibali.

Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search