Friday, 2 February 2018

Zari Kiboko Ampa Ujumbe Huu Mama Diamond

 Mmh! Zari Kiboko Ampa Ujumbe Huu Mama Diamond “Fanya tuhame Guest House tumuachie mwanao”
Bado inaonekana ishu ya Diamond Platnumz kudaiwa kulala na wasichana wengine nyumbani kwake Madale, mama watoto wake Zari The Boss Lady hajaichukulia poa na inadaiwa kuwa amekasirishwa na tuhuma hizo zilizosambaa katika mitandao ya kijamii.

Diamond siku kadhaa zilizopita alidaiwa kupeleka msichana mwingine na kulala nae nyumbani kwake Madale, ila baada ya kuenea kwa video clip ikimuonesha msichana huyo akiwa Madale, Zari alionesha kukasirishwa na kuandika snapchat “Ati Madale State lodge au Madale Guest house?”


Baada ya siku kadhaa kupita baadhi ya mashabiki waliamini inawezekana ishu hiyo imepita ila comment ya Zari katika post ya instagram ya mama Diamond inaonesha amekasirika bado, hiyo ni baada ya ku-coment katika picha ya Mama Diamond aliyopost na kuandika “Kubwa la maadui” ikimuonesha Mama Diamond akiwa Madale lakini Zari akacomment “Fanya tuhame Guest House tumuachie mwanao”

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search