Friday, 2 February 2018

ZITTO KABWE DENI LA TAIFA LIMEONGEZEKA

Image result for zitto kabwe

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa deni la taifa limeweza kuongezeka kwa asilimia 168% ndani ya muda mfupi toka Serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani.

Zitto Kabwe amesema hayo Januari 1, 2018 wakati akichangia Bungeni na kudai kuwa kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad ndani ya kipindi kifupi deni la taifa limeongezeka. 

"Ukitizama aliyosema CAG kuhusu deni la taifa inaonyesha kwamba ndani ya kipindi kifupi sana deni la Taifa limeongezeka kwa asilimia 168% lakini baya zaidi deni ambalo linatokana na masharti ya biashara limeongezeka kwa asilimia 17 ndani ya mwaka mmoja, madeni yanayotokana na masharti ya biashara gharama zake ni kubwa sana na inawezekana uwezo wetu wa kuyalipa ukawa na matatizo makubwa sana. Ndani ya taarifa hii ya CAG inaonesha kwamba taarifa ambayo Serikali ilitoa kuhusu deni la Taifa, deni la jumla ya tilioni 3.2 halikuwepo kwenye taarifa ya deni la Taifa, tulitarajia leo tungepata maelezo kwanini tilioni 3.2 hazikuhusisha katika taarifa ya pamoja ya deni la Taifa" alisema Zitto Kabwe 

Mbali na hilo Zitto Kabwe alimjia juu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Naibu wake kwa kitendo cha kuwadanganya wananchii juu ya ujenzi wa reli mpya wa kisasa Standard Gauge kwa kusema inajengwa kwa fedha za ndani ili hali Serikali inakopa fedha ili kujenga reli hiyo. 

"Serikali imekamilisha majadiliano na taasisi za kifedha kwa lengo la kukopa kiasi cha dollar za Marekani Bilioni 1.5 kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha 'standard gauge' kutoka Morogoro hadi Makutopora Serikali inakamilisha utaratibu wa kusaini mkataba. Waziri Mpango ruhusa uliyopewa na Bunge ni kukopa dollar za Marekani Milioni 700 ni wapi ulipata ruhusa ya kwenda kujadiliana kukopa ziada ya 1.5 Bilioni ?

Zitto Kabwe aliendelea kuhoji

"Wabunge wote humu ndani ni mashahidi kila siku tunaambiwa, tunajenga reli ya Standa gauge kwa fedha zetu za ndani lakini leo Serikali inasema tunakopa, Kwanini tunawalaghai wananchi? Kwanini hatuwaelezi wananchi ukweli kwamba hatuna uwezo wa kujenga kwa fedha za ndani lakini tunakopa, kuna ubaya gani maanake kukupa si dhambi, kwanini tunamuacha Rais anasema tunajenga reli kwa fedha zetu za ndani halafu tunakuja Bungeni taarifa za Serikali zinasema kwamba tunakopa mnamuaibisha Rais" alisisitiza Zitto Kabwe 


Jana nilizungumza Bungeni kuchangia mjadala wa Ripoti za Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), mchango wangu ulijikita katika Mambo matatu muhimu yafuatayo:
Kuhusu Ripoti ya PAC
1. Deni la Taifa: Deni limekua kwa zaidi ya 168%, kwa mwaka mmoja tu Mikopo ghali (ya Kibiashara) imekuwa kwa zaidi ya 17% (na hivyo 31% ya deni la Taifa kuwa ni Mikopo ghali). Tutateseka sana kulipa.
2. Wakati wa kuwasilisha Bajeti ya 2017/18 Serikali iliomba Bunge ruhusa ya kukopa $700 milioni (takribani Trilioni 1.5). Lakini taarifa ya miezi 6 ya Utekelezaji wa Bajeti inaonyesha Serikali inakopa $1.46 bilioni (takribani trilioni 3), mara 2 ya fedha ilizoomba na kuidhinishiwa na Bunge. Hii ni kinyume na utaratibu.
3. Takukuru hawajafunga hesabu tokea mwaka 2016. Sheria iliyounda Takukuru inawataka wafunge hesabu, wakaguliwe na CAG na mahesabu yao kuletwa Bungeni. Taasisi inayozuia rushwa lazima iwe mfano wa kufuata sheria, hasa katika wakati ambao wamemshataki Mhasibu wao kwa Ufisadi.
Kuhusu Ripoti ya LAAC
4. Kila mwaka tunapaswa kutoa 10% ya Mapato ya ndani ya Halmashauri kama mikopo kwa wanawake na vijana. Kwa mwaka huu 10% hiyo ni zaidi ya Bilioni 60, tuziwekee utaratibu kwa kuzianzishia benki ili kwanza Halmashauri zitoe fedha hizo, ziokopeshwe kwa Vijana na wanawake kupitia vikundi, na benki husika iwezeshe mikopo hiyo kurejeshwa. Na Vikundi viungwe kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
5. Land for Equity: Kuna maelekezo ya Kila Mkoa kuwa na Viwanda 100, uwekezaji umilikishe uchumi kwa watu wetu, tuache kulipwa fidia, tupewe hisa kwa ardhi tunazotoa kwenye ujenzi wa viwanda kwa utaratibu wa Land for Equity. Mradi wa Hospital kubwa ya Kigoma Ujiji kwa utaratibu huu utatupa bilioni 5 kwa mwaka kwa hisa zetu 20% zinazotokana na mtaji wa ardhi tunaoutoa. Waziri wa Tamisemi alilete jambo hili kisheria, ili lifanyike na kwenye Halmashauri zingine.

r

Habari kwa hisani ya EATV
CREDIT:JAMII FORUM

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search