Monday, 12 March 2018

Ajali ya ndege nchini Nepal yasababisha vifo vya abiria 40

media

Ndege ya abiria iliyoanguka ikiteketea moto katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Kathmandu nchini Nepal Machi 12 2018
Watu 40 wameuawa na 23 kujeruhiwa baada ya ndege ya abiria ya  Bangladesh iliyokuwa na abiria 67 kuanguka wakati ikitua katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Kathmandu nchini Nepal.Maafisa nchini Nepal wanasema abiria 17 waliokolewa baada ya ajali hiyo huku wengine wengine wakipoteza maisha.
“Watu 31 waliuawa papo hapo na wengine tisa wakapoteza maisha wakiwa hospitalini jijini Kathmandu,” amesema msemaji wa Polisi Manoj Neupane.
Ndege hiyo ilikuwa imetokea jijini Dhaka, ikielekea jijini Kathmandu.
Moto mkubwa na moshi mzito ulishuhudiwa pindi tu ndege hiyo ilipoanguka na maafisa wamekuwa na kazi ngumu ya kujairbu kuuzima ili kuona iwapo itawaokoa abiria.
Uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali ya ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Marekani, US-Bangla.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search