Friday, 23 March 2018

ALIYETEKA NDEGE YA TANZANIA MWAKA 1982 KUMTAKA NYERERE AJIUZULU AFARIKI

 
Wakili nguli Yasin Memba anayedaiwa kuteka ndege ya Tanzania mwaka 1982 amefariki dunia jana Jumanne Machi 20, 2018 jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.Kwa mujibu wa wakili wa kujitegemea na mwanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS) Mathew Kakamba, amesema Memba amefariki dunia katika Hospitali ya Aga Khan na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini humo.


Memba ni miongoni mwa watanzania wawili wanaodaiwa kuteka ndege ya Tanzania iliyokuwa na abiria 90, Februari 1982 wakishinikiza Rais wa wakati huo, Julius Nyerere kujiuzulu.

Chanzo - Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search