Wednesday, 21 March 2018

BABA ACHIMBA KABURI USIKU KISHA KUMZIKA MWANAE AKIWA HAI

Polisi wa Migori nchini Kenya wanachunguza kifo cha mtoto mwenye umri wa miezi 6, ambaye inasemekeana alifukiwa akiwa hai na baba yake mzazi.

Kwa mujibu wa kiongozi wa eneo hilo Chief Fredrick Owino, mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la Marcellus Odek, alirudi nyumbani kwake akiwa amelewa na kuchukua jembe na kuchimba kaburi, ambalo alimzika mtoto huyo ambaye ameelezwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kupumua.

Taarifa zaidi zinasema kwamba mama wa mtoto huyo Annah Auma wakati tukio linatokea alikuwa amepoteza fahamu kutokana na tatizo la kifafa alilokuwa nalo, na alifanya tukio hilo mbele ya familia yake na majirani, usiku wa Machi 14 mwaka huu.

Ndugu wa familia hiyo Milicent Achieng amesema mtuhumiwa aliwakuta nyumbani na mtoto akiwa anapumua, kabla hajaanza kuchimba kaburi na kumfukia, na alipoomba msaada kwa watu walikataa na kumshauri akimbie kwani huenda angemuua na yeye.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search