Thursday, 29 March 2018

Balozi Jack Zoka kurejea, awaaga Canada; Magufuli kuamua mrithi wake

zokas.jpg 

Balozi wa Tanzania nchini Canada aliyemaliza muda wake, Jack Mugendi Zoka, amekwishaagana na Watanzania wanaoishi nchini humo, na atarejea hapa nyumbani (Tanzania) Machi 31, wiki hii, mtandao wa huu wa www.tanzanianewsroom.com umebaini

Jack amekwishaagana na Watanzania wanaoishi nchini Canada Machi 17, mwaka huu, na zaidi ya hapo, ameandika barua ya kuwashukuru, shukurani ambazo amezihusisha pia na mkewe, Esther Zoka. Na kwa sasa, Rais John Magufuli ndiye mwamuzi wa nani anakwenda kuchukua nafasi hiyo ya Zoka nchini Canada, ambako ndiko Tanzania imefanya biashara ya ununuzi wa ndege za Bombardier.

“Kwa mara nyingine tena napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru nyote kwa ushirikiano ambao mmekuwa mkinipa tangu nilipofika Canacda mwezi Februari 2015.

“Katika kipindi cha miaka mitatu nimejitahidi kuwa na mawasiliano ya karibu nanyi ingawa kutokana na ukubwa wan chi hii, sikuweza kuwafikia nyote, lakini kutokana na maendeleo ya teknolojia pamekuwa na mawasiliano ya kila mara.

“Kama Balozi wa Tanzania katika eneo langu la uwakilishi, moja ya majukumu yangu muhimu yamekuwa ni kuwafikieni wana-diaspora kwa njia mbalimbali ili kwa kushirikiana nanyi tutoe mchango wenye tija kwa masilahi ya maendeleo ya nchi yetu, Tanzania.

“Nataraji kuondoka Canada tarehe 31, Machi 2018 kurejea nyumbani. Nina imani ushirikiano huu mzuri niliopata kutoka kwenu mtautoa pia kwa balozi atakayekuja kuchukua nafasi niliyokuwa nayo. Kwa wale mtakaopata fursa kuja Tanzanai, karibuni sana nyumbani.


Chanzo: Tanzanite times

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search