Wednesday, 21 March 2018

DIAMOND-HAKUNA MWANAMKE ALIYENILIZA KAMA WEMA

Mapenzi ni matamu kuzidi asali, lakini ukitendwa huwa machungu zaidi ya shubiri. Diamond Platnumz amemtaja mrembo ambaye amewahi kumtoa chozi wakat wapo kwenye mahusiano.


Diamond amefunguka na kueleza ya moyoni mwake ambapo amekiri kuwa hakuna mwanamke ambaye alikuwa kumliza kwenye mapenzi kama Wema Sepetu.


Diamond amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya nchini Kenya na Citizen Radio na Willy .M. Tuva, ambapo amedai Wema ni mwanamke ambaye alimtambulisha sana machozi.


"Mara ya mwisho kulia kwa sababu ya mapenzi ni nilivyokuwa na uhusiano na Wema Sepetu dah yule mwanamke ameniliza sana hadi nakumbuka kuna siku nilikuwa pale home nipo gym babu Tale akawa ameona kuna maambo mabaya mabaya mtandaoni akaniambia mdogo wangu si uachane naye? Mi nakumbuka nikamwambia yaani sikudanyi bosi yule mwanamke nikiwa naye najisikia kama niko peponi kwaiyo hata tulivoachana alikuwa haamini”.


Lakini pia Diamond amesisitiza kuwa ni kweli amemwagana na Zari na wala sio kiki kama watu wengi wanavyodai ila amesema kwa sasa hataki kumuongelea Zari kwani ameelekeza nguvu zake kwenye kuitangaza albamu yake iliyotoka siku chache zilizopita.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search