Wednesday, 21 March 2018

Diwani wa kata ya Kaloleni Arusha kupitia CHADEMA ajiuzulu udiwani

Arusha.Diwani wa CHADEMA Kata ya Kaloleni jijini Arusha, Emmanuel Kessy amejiuzulu uanachama wa chama hicho na kujiunga CCM huku akitoa sababu tatu za uamuzi wake huo.

Diwani huyo alitangaza kujiuzulu jana usiku Machi 19, 2018 na kufanya idadi ya madiwani wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini wanaohamia CCM kufika takribani 46.

Akizungumza leo Jumanne Machi 20, 2018 na MCL Digital, Kessy amesema moja ya sababu hizo ni kumuunga mkono Rais John Magufuli aliyedai kuwa anapambana vyema na rushwa, ufisadi na kuwaletea maendeleo wananchi.

Sababu hiyo pia, imekuwa ikitolewa na madiwani wengi wa CHADEMA wanaohamia CCM

Amesema sababu nyingine ni kupunguza msuguano uliopo baina yake na viongozi wa CHADEMA.

Pia, amesema ana imani na CCM na kwamba akiwa ndani ya chama hicho kutarahisisha utendaji wake wa kazi.


Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search