Monday, 12 March 2018

FLORA MBASHA AMJIBU EMMANUEL MBASHA KUHUSU MTOTO

Msanii wa nyimbo za Injili Flora Mbasha ambaye alikuwa mke wa mwanamuziki wa Injili Emmanuel Mbasha, amefunguka juu ya kitendo cha aliyekuwa mume wake kumlalamikia kumnyima mtoto kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv, Flora Mbasha amesema hawezi kulizungumzia suala la hilo kwenye vyombo vya habari au kwenye mitandao, kwani yeye ndio anaujua ukweli, na iwapo mahakama ilimpa haki ya kumuona mtoto, kuandika kwenye instagram sio sahihi kwani mahakama haipo instagram.

“Siwezi kulizungumzia suala hilo kwenye vyombo vya habari, hilo suala kama aliandika kwenye instagram nami jibu ningelitolea instagram, na ukweli hamuujui sisi ndio tunaujua, na kama mahakama iliamua hivyo, na yeye kuandika instagram, kama mahakama iko instagram basi sawa acha aandike, ila siwezi kuliweka wazi”, amesema Flora Mbasha.

Wawili hao walitalikiana baada ya kesi aliyokuwa akituhumiwa Emmanuel kuisha na kukutwa hana hatia, na kisha Flora kuolewa na mwanaume mwengine. 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search